Mapenzi huanzia katika familia yako

Mapenzi huanzia katika familia yako

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
461
Reaction score
392
Mama mmoja aliewalea watoto wake kwa taabu sana na wakawa wamefanikiwa kimaisha ingawa wote walikuwa hawamkumbuki, siku moja alipatwa na na tatizo akiwa shambani na kuvunjika miguu yote miwili.

Kwa haraka ikabidi awaombe waliokuwa wakimuuguzia nyumbani watoe taarifa kwa vijana wake wapendwa ili waje japo kumpa fedha ili atibiwe na kuweza kuwa mzima tena.

Baada ya kulazimishwa sana wale watoto waende kumwangalia mama yao, mmoja wao akaamua aende ili kumaliza kelele za ndugu na wengine kuendelea kuta bata huko walipo.

Akawasha gari yake aina ya Jeep na kwenda mpaka huko mkoani Mbeya. Kufika pale mama alifurahi sana na kumwambia mwanawe kuwa alihitaji msaada wake kwani bado alihitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi ingawa alishindwa fedha.

Yule kijana kwa dharau na jeuri aliyokuwa nayo alisema, " mama wewe ushazeeka sasa na tatizo hili limekufanya uwe kiwete hivyo sioni haja ya wewe kumaliza fedha kwa matibabu, bali wewe baki hapa hapa umalizie siku zako za kuishi"

Yule kijana alimaliza na kuwasha gari akiondoka zake huku akimwacha mama yake machozi yakimtoka na baadhi ya ndugu wamemshikilia wakimsihi amsamehe tu Yule mtoto kwani hajui alitendalo.

Jioni ya siku ile Yule kijana akiwa ametoka bar kunywa ili akijiandae kwa safari yake ya kurudi dar, alipatwa na ajali mbaya sana ambayo mpaka sasa imemfanya ashindwe kutembea wala kufanya chochote kwani alivunjika mgongo.

Na kwa kuwa yeye pekee ndiye aliyekuwa akiwasaidia wenzake katika biashara zao basi wadogo wakashindwa kusimamia biashara na mpaka hivi sasa wote wako kijijini wakimtegemea mama yao ambaye wasamaria wema walimsaidia mpaka anapona miguu yake.

JAMANI, Kabla hujafa hujaumbika na kumbuka upendo wa mama hauna kikomo, kwani mama Yule aliyeambiwa kuwa ni kiwete na angekufa MAPEMA, leohii yeye ndiye anamhudumia Yule kijana ambaye ni wakumalizia haja zote sehemu alipo.

Na kama haitoshi wale wanawake wazuri aliokuwa nao pamoja na marafiki wote wamemkimbiana sasa kimbilio lake ni kwa mama yake tu.

Mkumbuke mama yako siku ya leo kwa kusema "NAKUPENDA MAMA" kama kweli unamjali

 
watoto wa siku hizi ndivyo walivyo!

kuna watu wana elimu zao nzuri tu, lakini hawajitambui kabisa linapokuja suala la wazazi wao! matunzo ya wazazi ni jukumu la mtoto.. no matter what happens..
 
Niwe na uwezo wote huo nishindwe kumtunza mzazi wangu.. !
 
Nakupenda sana mama yangu wala sina mama mwinginge zaidi yako.
 
Tuwapende/tuwajali/tuwanyenyekee wazazi wetu
 
kweli unampenda mama yako na kama kweli basi muombee mama yako maisha marefu na kama hayupo duniani
basi muombee kwa mungu apumzike mahali pema peponi amiiiiiin
 
My mom ndio kila kitu kwangu, namshukuru kwa kunifikisha hapa nilipo, RIP my mama nakupenda but Mungu alikupenda zaidi! Will love you ever mom kwani sijapata mbadala wako hadi leo
 
Leo kuna habari za makalio tu. Haya mengne badae.
 
Back
Top Bottom