Mapenzi hayalazimishwi Usifurahie maisha mabaya ya Ex wako

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Habari zenu Wakuu,

Nimekuwa nikiona nyuzi nyingi sana za wanaume wenzangu wakifurahia Maex zao kuharibikiwa na maisha baada ya kuachana kwao.

Nikajaribu kuchunguza na nikagundua kwamba, hao wanaume walivyoachana/walivyoachwa na wanawake zao waliumia ndio maana wanafurahia anguko baya la maex zao wa kike.

USHAURI
Wanaume wenzangu Mapenzi huwa hayalazimishwi yanakujaga tu yenyewe automatically bila ya kufosiwa, Mwanamke anapoachana nawewe shukuru na songa mbele acha kuweka vinyongo na visasi kwa mtu ambaye hakupendi na wala hawazi lolote kuhusu wewe.

USILAZIMISHE KUPENDWA, JIPENDE WEWE MWENYEWE
 
Kazi kweli kweli / job true true

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Nimeibeba hii mada kiujumla. Kiubinadamu, mtu aliyekukosea, mliepishana, mliyevurugana in the past, ukaja kumuona katika dhiki, huwa tunasuuzika na kufurahia mateso ya mtu huyo. Lakini nimekuja kugundua its very bad, na huwa inaonyesha vinyongo na visasi tulivyovibeba enzi na enzi. Kuna mfano ndani ya biblia, Yesu alipofika kwenye msiba wa kijana, akakuta watu wanaomboleza. Akawaambia hajafa huyu, wakamcheka sana kwa dhihaka. Yesu akaingia, akamponya kijana, kijana akafufuka. And guess what..Jesus slipped through the backdoor. Ile ni act kubwa ya humility.

Na sisi wafuasi wake, tunatakiwa tuwe kama yeye. Tujifunze kupita mlango wa nyuma. Tusitafute recognition, sifa kwa wanadamu. Kuna ile tunamwambia mtu "nilikwambia, ona sasa, ukome, safi sana" apatwapo na madhila. Na hii huwa inaleta a sense of satisfaction kwenye mioyo yetu idanganyayo. Lakin hii tabia sio unyenyekevu.

Ukitaka kujipima kama umesamehe, jisachi nafsini mwako kwa haya maswali; Je ukimuona aliyekujeruhi once in life amepatwa na kubwa la dunia how do you feel? Unatamka nini moyon mwako? Je unaweza kumuombea, kumuosha miguu (an act of service) aliekuumiza? Unaweza kufunga na kumuombea pale Bwana anapokuletea assignment? Unaweza kumuuguza hospitali kama mtoto umpendae? Na mambo kama hayo. Kibinadamu ni ngumu sana, lakin kwa Mungu yote yanawezekana. Tukiamini. #Loud thoughts#
 
😂😂😂 umenikumbusha mbali sana phina wangu nilikuwa nampenda mnoo,dem alikula pesa yangu sanaa halafu akaja nimwaga ghafla kuchunguza kuna fundi garage mchundo kanizidi kete kwa pesa za wizi wa vipuri vya kachomoa kwa magari ya watu, mwisho wa siku akaja gundulika akafukuzwa na mwenye garage, pesa za kumhudumia phina zikakata ghafla bin vuuu siku moja mimi na phina tupo ndani ya daladala moja, binti kajchuja ile mbayaa na mtoto kazalishwa, tako limeporomoka, nyonyo imekuwa kandambili, huruma ilinijia lakini nikikumbuka alivyonitesa kwa mineno ya shombo nikajikuta nafurahi na kujisemea karma is real
 
Nimeibeba hii mada kiujumla. Kiubinadamu, mtu aliyekukosea, mliepishana, mliyevurugana in the past, ukaja kumuona katika dhiki, huwa tunasuuzika na kufurahia mateso ya mtu huyo. Lakini nimekuja kugundua its very bad, na huwa inaonyesha vinyongo na visasi tulivyovibeba enzi na enzi. Kuna mfano ndani ya biblia, Yesu alipofika kwenye msiba wa kijana, akakuta watu wanaomboleza. Akawaambia hajafa huyu, wakamcheka sana kwa dhihaka. Yesu akaingia, akamponya kijana, kijana akafufuka. And guess what..Jesus slipped through the backdoor. Ile ni act kubwa ya humility.

Na sisi wafuasi wake, tunatakiwa tuwe kama yeye. Tujifunze kupita mlango wa nyuma. Tusitafute recognition, sifa kwa wanadamu. Kuna ile tunamwambia mtu "nilikwambia, ona sasa, ukome, safi sana" apatwapo na madhila. Na hii huwa inaleta a sense of satisfaction kwenye mioyo yetu idanganyayo. Lakin hii tabia sio unyenyekevu.

Ukitaka kujipima kama umesamehe, jisachi nafsini mwako kwa haya maswali; Je ukimuona aliyekujeruhi once in life amepatwa na kubwa la dunia how do you feel? Unatamka nini moyon mwako? Je unaweza kumuombea, kumuosha miguu (an act of service) aliekuumiza? Unaweza kufunga na kumuombea pale Bwana anapokuletea assignment? Unaweza kumuuguza hospitali kama mtoto umpendae? Na mambo kama hayo. Kibinadamu ni ngumu sana, lakin kwa Mungu yote yanawezekana. Tukiamini. #Loud thoughts#
Well well well said mkuu nimependa maneno yako
 
Ukipigwa na kitu kizito kwenye mahusiano kuachilia inahitaji moyo wa hekima ya juu sana .Binafsi niliumizwa na Ex wangu Ila namtakia mafanikio huko aliko🙏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom