Beesmom
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 37,365
- 91,926
Unakuta msichana mdogo tu kavaa kitenge, kanga, gauni bwanga kama anazuia mimba isionekane, yaan hivyo vyote kavaa kwa pamoja na remba kichwani na yeboyebo au skuna. Ukiuliza unaambiwa ndo vaa yake tangu aolewe na yule mbaba. Yaani kujivika kote huko manguo ili aonekane MTU mzima na kupunguza aibu za kuongozana na huyo waliyezidiana 25 yrs.
Mmama nae na 45 yake kavaa kimini kimembana mpaka unatamani umtafutie oxyg aongezewe hewa apumue vyema, na kitop cha haja apo tumbo limezidi nguo ivo laning'inia na mchuchumio juu, na tinted kabisa kisa tu afanane kidogo muonekano na huyo 21 boy wake.
Kijana mkaka sasa, ndo tobaa, hiyo suruali ya kitambaa ukubwa wake ule mfuko wa mashineni unauhafadhali, shati pepe kale akabane kwa Fundi, viatu vimempwaya ili tu afanane muonekano na 56 mom wake.
Siteseki ila naona mnateseka kujinyima uhuru. Ukiamua kudate na mliyezidiana kimwonekano embu baki kwenye umri wako, la sivyo tutafute size zetu aisee.