Jamani mimi sina mengi zaidi ya kukipongeza kiwanda kinachotengeneza kilevya aina K-Vant.
Niwe muwazi kinywaji hiki kinafaa sana kulingana na maoni na mawazo ya watumiaji tumekipenda sana ila tunapendekeza yafuatayo:-.
1. Kama kuna madhara ya kibinadamu/kiafya tafuteni namna ya kuyaondoa sio kuyapunguza (yaondoeni kabisa)
2. Kama haiwezekani kuyaondoa madhara yotokanayo na utumiaji K-Vant, wateja wenu tunaomba mtupe elimu ya kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kwa watumiaji wanaozidisha matumizi ya K.Vant kupita kiasi yaani (excessive consumption of K-Vant), pia toeni ushauri ni kiasi gani tunywe kulingana na afya zetu Kumbukeni nikinywa zaidi ya uhalisia nitapoteza fahamu ndio maana huwa tunaahidi Murano wakati hata uwezo wa baiskeli hatuna.
K-Vant ni kilevya ambacho tumekipenda wengi je kiafya kina mdhara gani?. JF pombe sio maji sio maji tafakari chukua hatua.