Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na mijadala mbalimbali inayohusu idara ya usalama Tanzania ijulikanayo kama TISS.
Mijadala hiyo imeelekezwa zaidi kwenye kuishutumu idara hiyo kwa kujishughulisha zaidi ya ukandamizaji wa haki za binadamu na kuwadhibiti wapinzani wa serikali inayoongozwa na chama tawala cha CCM.
Mimi, binafsi lazima niseme ukweli, nimependezwa sana na kasi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali na sekta mbalimbali nchini mwetu.
Pia nimependezwa na juhudi za raisi John Magufuli kuisimamisha Tanzania kwenye ramani yake halisi barani Afrika na kwingineko.
Nimekuwa namuunga mkono raisi Magufuli katika michango mingi humu JF na kila mara nimekumbana na kasi kubwa ya mashambulizi kutoka kwa wanachama wenzangu ambao (kwa mtazamo) wao wanaona raisi John Magufuli anakosea kwenye baadhi ya mambo hususani uendeshaji wa idara ya usalama wa taifa ya TISS.
Ni juzi tu raisi Magufuli amemteua bwana Diwani Athumani kuwa mkurugenzi mkuu wa TISS uteuzi ambao si tu umenistua bali pia umeiacha na masuali mengi.
Masuali hayo pamoja na mengine ndo yamenisukuma kuandika haya maoni khasa kwenye eneo la uteuzi na kwamba kuna haja ya TISS kuundwa upya na pia uteuzi wa mkurugenzi mkuu kuwepo na nafasi ya Bunge letu tukufu kupitia sifa za mteule mpya wa TISS na kumthibitisha kabla ya kuapishwa rasmi na raisi.
Mimi pia ni mdau tu hivyo maoni haya yasichukuliwe kuwa ni kuingilia shughuli za idara hiyo bali ni kupeana ushauri na mapendekezo yanayolenga kuilinda nchi yetu katika masuala yote yanayohusu maslahi yake, uchumi wake na nyanja zingine muhimu.
Update: 12/04/2021
Raisi Magufuli RIP hatunae tena, alitangazwa kufariki tarehe 17 March 2021.
Sasa hivi tunae raisi Samia Suluhu Hassan ambae alikuwa ndie ataongoza serikali ya awamu ya tano kumalizia miaka minne ya mwisho ndani ya awamu mbil hadi 2025.
Twende kazi.
Mpaka sasa sheria ya usalama wa taifa ni ile ya mwaka 1996 ambayo inaelezea muundo wa TISS kama idara chini ya ofisi ya raisi.
Ushauri ni kwamba sheria inayounda TISS ipitiwe upya na ikiwezekana kuwe na sheria mpya kabisa ya kuundwa kwa idara hii na vitengo vingine ndani yake vitakavyokuwa na majukumu tofauti ya TISS.
Sheria hiyo mpya itakuwa inafafanua wazi kwamba TISS ipo kwa ajili ya maslahi ya taifa na usalama wake, uchumi wake na raia wake. na ipo kuzuia hujuma dhidi ya taifa letu, ugaidi, na vitendo voyote vinavyohatarisha usalama wa nchi na shughuli za kimaendelao na demoktasia kwa ujumla.
Hivyo basi, TISS haitaonekana kwamba ipo kwa ajili ya chama taala pekee bali ni kwa kila mtanzania.
Yaani: TISS ni Usalama wa taiifa chini ya mkurugenzi wake mkuu na mitandao yake yote nchi nzima.
Mkurugenzi wake mkuu ateuliwe na raisi lakini aidhinishwe na Bunge kwa sababu katika nchi zingine huyu bosi ana level moja na waziri yoyote yule yaani anakaa kwenye kikao cha BLM.
Akiidhinishwa Bunge anakuwa amepitia chujio.
Huyu DG anakuwa kama inavyojulikana anatoa PDB (taarifa za kila siku) kwa raisi kila usubuhi na hii PDB huwa inatoka kwenye idara zote nchi nzima na hata nje.
Hivyo, DG wa TISS aiongoza na kuielekeza TISS kwenye masuala na mpango mzima wa Usalama wa Taifa na pia ni mshauri wa raisi kama nilivyosema hapo juu kuhusu PDB.
Itaendelea, ntaongelea mapendekezo ya TISS mpya na vitengo vyake kikiwemo kitengo cha ujasusi wa nje ya Tanzania , maana suala la kuzuiwa ndege yetu ya ATCL kule Afrika Kusini limetutia aibu sana.
Pia ntaongelea tofauti yake na polisi lakini uwiano wake wa kazi na JWTZ.
Pia ntaongelea nini maana ya jumuiya ya wanausalama na umuhimu kwake kwa taifa la Tanzania linaloelekea kwenye hatua ya kila mwananchi kupata maziwa na asali.