Mapendekezo Fao La Kujitoa kutua Bungeni

Mapendekezo Fao La Kujitoa kutua Bungeni

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Tanzania Daima, linaripoti kuwa, mapendekezo kuhusu fao la kujitoa kutua bungeni.

Ukimsikiliza Mheshimiwa Mavunde katika maelezo yake kwa mbunge aliyetaka kufahamu juu ya fao la kujitoa ni kwamba, suala hilo lipo mbioni kufikishwa bungeni. Anaongeza Mheshimiwa waziri kwamba, serikali inatafuta namna nzuri ya kuwalipa wanaopoteza ajira kabla ya kufikisha umri wa miaka 55 au 60.
Je, wakati wao wakipanga haya mambo, kwa kipindi hiki ambacho kuna watu wameshapoteza ajira inakuaje? Je, watu waliopoteza ajira waendelee kutaabika wakati wao wakipanga mambo yao? Na kwa nini waliopoteza ajira kwa sasa wasiruhusiwe kuchukua pesa zao kwanza wakati wao wakipanga yao?---Haya ni maswali ambayo waheshimiwa wabunge ilitakiwa kimsingi waulize, lakini, no body cares! Vyama vya wafanyakazi nao, they don't care, it's like everything is fine, na hakuna kinachoendelea? Jamani, hivi kuna nini nchi hii? Hivi vyama vya wafanyakazi vinavuna pesa za wanachama wake kila mwezi, tena nyingi tu. Sasa kwa nini hawachukui hatua madhubuti kuwatetea wanaofanya waitwe viongozi wa trade unions, kwa nini hawawatetei wanaofanya walipane mishahara na posho mbalimbali....Enyi TUCTA....mpo kweli nchi hii au mpo nje ya Tanzania? Hivi hamuoni kuwa watu wanaumia mitaani?




faolakujitoa.JPG

 
Sisi hatutaki huo mswaada, hiyo ni dhuluma kwetu sisi masikini, ibaki vilevile ilivyokuwa
 
Kama wao hawataki kupangiwa basi nasisi wasitupangie,hela ni zetu kwa jasho letu.
 
mwenyezi mungu ni msikivu wa kilio cha wengi...
tusilazimishne jamani na hilo fao,ni dhuruma ya mchana kweupe kabisa....
 
Tena ccm waaache kuchezea watz....Wawatetee wanyonge kwa vitendo sio kununua ndege, kujenga chato ndo ionekane kutetea wanyonge...
HILI LA FAO LITAUA SN WATU
 
Tena ccm waaache kuchezea watz....Wawatetee wanyonge kwa vitendo sio kununua ndege, kujenga chato ndo ionekane kutetea wanyonge...
HILI LA FAO LITAUA SN WATU
Kwa hiy Chato hakuna wanyonge. Acha wivu wa kike.
Wangejenga kwenu ungesema hayo kweli?
 
Huo mswaada ni wa kufutilia mbali. Na tunafuatulia hili jambo kwa makini, hatua kwa hatua, ili tujiridhishe namna dhulma inavotaka kuchukua hatamu.
 
Yaani nilikuwa nawaza sana kuhusu jambo hii.Ee MUNGU wape hekima wabunge wetu wa CCM ili tupate haki yetu
 
Kwa upigaji uliopo bongo na kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu nashauri fao la kujitoa lisiwepo badala yake fao la kumjali mfanyakazi katika kipindi anapokua hana kazi lifikiliwe namna!!...
 
Inauma sana milioni 15 zangu PPF naishia kuziona kwenye makaratasi tu.
Lkn ipo siku.
mbaya zaidi familia yako inakula ubwabwa+maharage, inauma sana mi Presidaaaa akisaini sitamchagua next selection akiaMungu
 
Yaani nilikuwa nawaza sana kuhusu jambo hii.Ee MUNGU wape hekima wabunge wetu wa CCM ili tupate haki yetu
Siku hizi wanamsemo 'maagizo kutoka juu'
Hivyo yawezekana kabisa Ccm kwa wingi wao wakaamua kugongelea msumari na fao la kujitoa likaondoshwa rasmi
 
Serikali ya wanyonge . Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Huyo Dogo Mavunde ametoka shule Na kulamba shafu hajui maisha Ni nini. Anafikiri maisha Yamo CCM tu . Nje ya ajira huwa kuna maisaha mengine mimi ninafanya migodini ninafanya kazi miaka 3 minne napumzika na chukua changu nainvest somewhere then narudi and then I do the same. Sasa wanaposema hivo siwaelewi Na July hii nimemaliza cont yangu Na Nsssf zipo million za kutosha. Tutaandana maana hii serikali inafanya mambo yasiyojulika kwa vitu vinavyojulikana. Hatukubali hela zetu zitumiwe Na watu wasiojulikana.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Kwa hiy Chato hakuna wanyonge. Acha wivu wa kike.
Wangejenga kwenu ungesema hayo kweli?
Kumbuka kuwa mama yako ni wa kike.......!!?? KEY BOARD ZA lumumba zinawasumbua sn mbwa nyie
 
Back
Top Bottom