Mapato VS Matumizi ya Serikali

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,721
515
Kwa kweli juhudi zinafanyika nyingi sana ambazo kwa ujumla malengo yake ni kuogeza pato la serikali na hatimaye kuwekeza sehemu ya mapato hayo ktk utoaji huduma za kijamii husani public goods (miundombinu, afya, elimu nk).

Nia ni njema ingawaje njia za kuhakikisha mapato ya serikali yanaongezeka zimekuwa si rafiki asilani hazisaidii kufikia malengo ya serikali zaidi ya kurudisha nyumba uchumi wa nchi (Biashara nyingi zinafungwa nk) Mh. Rais pia analitambua hili na hata hivi katibuni alikemea na kuwaasa TRA kujipanga vyema zaidi. Kwa sasa TRA BADALA YA KUHAKIKISHA BIASHARA ZINAFANYA KAZI ILI WAPATE KODI....wamekuwa wa kwanza kuwashauri wafanyabiashara kufunga biashara zao kutokana na sintofahamu ya kodi.

Naomba nishauri pamoja na juhudi zote zinazoendelea serikali itazame uwinano kati ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Inashauliwa kuwa na matumizi makubwa zaidi ktk miradibya maendeleo na si vinginevyo. Nafikiri ni wakati sasa tuwe na muundo wa serikali ndogo.....wabunge wawili kwa kila wilaya kuwa na bunge (lower house) na mwakilishi moja kila mkoa iiundwe upper house. Wizara chache kwa kuziunganisha zinazofanya majukumu yanayofanana mfano afya elimu, ustawi wa jamii, vijana kazi na ajira. Hizo zinaweza kuwa ni wizara moja. Vile vile Ulinzi mambo ya ndani nk....utaratibu wa msululu wa vyeo hauna tija. Labda nitoe mfano wa wazara ya kilimo. Inasemekana kilimo cha TZ sehemu kubwa ni wakulima wadogo na kwa hiyo wanatatumia jembe la mkono zaidi....haingii akilini kuna wizara ya kilimo big as it is....ina simamia na kuendeleza sera za kilimo cha kujikimu. Hivi ni rais au nani alikuwa anawaza tu hivi ukifuta say wizara ya kilimo tutapungukiwa na nini?? (Like significantly). Kwa kwa muundo wa sasa rest assured hatutapungukiwa na kitu. Itoshe kusema tunahitaji kuboresha mifumo tulionayo ili kuendana na maono na kasi ya rais.
 
Back
Top Bottom