mapato mechi ya simba na yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mapato mechi ya simba na yanga

Discussion in 'Sports' started by Mujumba, Mar 7, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAPATO MECHI YA YANGA v SIMBA

  Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom namba 108 kati ya Yanga na Simba lililochezwa jana (Machi 5) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 243,017,000 kutokana na watazamaji 46,539 waliokata tiketi kushuhudia.

  Maeneo ambayo tiketi ziliuzwa zote ni viti vya kijani 19,648 na viti vya bluu 17,045. Maeneo ambayo tiketi hazikuuzwa zote ni viti vya rangi ya chungwa (orange straight and curve), VIP C, VIP B na VIP A ambayo tiketi zilizouzwa ni 309 kati ya viti 748 vilivyopo.

  Viingilio katika mechi hiyo iliyooneshwa moja kwa moja (live) na Star TV na Super Sport 9 vilipangwa kama ifuatavyo; sh. 3,000 (viti vya kijani), sh. 5,000 (viti vya bluu), sh. 7,000 (orange straight and curve), sh. 10,000 (VIP C), sh. 20,000 (VIP B) na sh. 30,000 kwa VIP A.

  Baada ya kuondoa gharama za mchezo na mgao kwa uwanja, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kila timu ilipata mgao wa sh. 51,194,793.

  Boniface Wambura

  Ofisa Habari
  sasa haya mapato kwa club zetu nani anafaidika zaidi? na je tunaendeleza soka au?
   
 2. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  zaidi ya 50% ni chakula ya serikali na washirika,teh teh tehee hii bongo au hujui?
  hivi uliwahi kujiuliza kule oldi trafodi,darajani,nuuu camp mapato yanaendaje?
   
Loading...