Hawa wazenj ni watu wa ajabu sana, mambo yao yakiwa mazuri hawautaki muungano; kama wakati walipodanganywa kuwa mafuta yamegunduliwa huko kwao; lakini mambo yanapowachachia ndio wanakumbuka kuwa kuna big brother[ muungano] kwamfano sasa wanapopata taabu ya umeme. Nyiewazenj mkumbuke kuwa YOU CANNOT EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT!!
poa tu, muungano ufe.kabla ya muungano zanzibar ilikua poa tu...huu muungano wa kulazimishana hatuutaki...MUUNGANO WA KUTIANA NJAA...muungano na ufe,sie watanganyika tumeuchoka sasa,tuwaachie vijisiwa vyao tuone hayo maendeleo wanayoyaota period.
mimi sioni manufaa yeyote yale ya muungano...huu muungano unaiangamiza zanzibar...maendeleo ya zanzibar yemerudiswa nyuma miaka 30...watanzania amkeni,huu muungano unawanufaisha kundi l a watu fulani lakini waliowengi umewaletea taabu tu ya maisha...muungano ufe kila mtu aangalia mpango wake...watanzania amkeni...muungano wa kulazimishana sio muungano...poa tu cuf ishinde znz halafu wasimame kudai haki za zanzibar...hao wanaoongoza tanzania ,tanganyika imewashinda na sasa wanalazimisha zanzibar iingie katika janga lao la ufisadi. Bila ya muungano zanzibar ingekua mbali sana...toka vianze vyama vingi vya siasa, kumekuwa na uhasama mkubwa kati ya ccm na cuf kwa upande wa znz. Kwa mtazamo wa wengi, uhasama huu umesaidia kwa upande wa bara kwa sababu wa znz badala ya kudai haki zao za msingi kutoka bara wamekuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Wakati mwalimu nyerere yuko hai, wa znz walikuwa wakimuogopa sana, lakini toka amefariki na hofu yao imeondoka. Nimesafiri nchi nyingi sana, watu wengi kutoka europe, asia na america hawaijui tanzania, lakini wanaijuwa znz kutokana na historia yake. Watalii wengi wanakuja tanzania kutokana na umaarufu wa znz duniani. Neema kubwa tunayopata tanzania inatokana na kuweko kwa huu muungano. Hofu kubwa inayojitokeza ni kuwa endapo cuf na ccm wataelewana huenda ikapelekea wakadai haki zao nyingi ambazo upande wa bara wamekuwa wakiziminya, na hii inaweza pia ikaleta mvutano ambao ukasababisha kuvunjika kwa muungano!.. Wana jf mawazo yenu yanakaribishwa
hakuna mzeji hata mmoja anaetaka muungano...na huo umeme wa tanesco haupelekwi buru zanzibar...hii ni biashara tanesco wanauza umeme zanzibar...kabla ya hapo zanzibar umeme ulikuwepo...kwahiyo huu umeme isiwe sababu ya kuitawala zanzibar...muungano uvunjike kila mtu aangalie mpango wake...muungano=ngaa,taabu na maisha mabovu...hawa wazenj ni watu wa ajabu sana, mambo yao yakiwa mazuri hawautaki muungano; kama wakati walipodanganywa kuwa mafuta yamegunduliwa huko kwao; lakini mambo yanapowachachia ndio wanakumbuka kuwa kuna big brother[ muungano] kwamfano sasa wanapopata taabu ya umeme. Nyiewazenj mkumbuke kuwa you cannot eat your cake and still have it!!
Pindi mtoa mwana JF aandikapo hapa ukumbini, cha kwanza mimi nathamini zile dakika 2...3...... alizozitumia hapa ukumbini. Na kwa mantiki hiyo, leo napenda kukupongeza kwa muda ulioutumia hapa JF, na sio kwa hoja ulizozitoa. Kwani hoja zako ni dhaifu sana.Usipoteze muda wako kwa siasa za CUF na CCM , ni vyema ukahangaikia fungu lako la muhogo ule na wanao swala la Seif na Dr Karume halina maslahi si kwa wa Tanzania bara wal Visiwani. Shida yetu ni Umeme, Elimu bora na si mradi bora Elimu, maji safi na salama, huduma za afya na mawasilano bora na ya kudumu ikiwemo na swala la ajira.Haya ndiyo mambo ya msingi kwa wa Bongo siyo kuomba msaada kwa pengo kuunga mkono upuuzi, ni vyema ukawashauri hao viongozi wako wa dini wazid kuwapigia kelele serikali ya Bw Kaujanja-Kikwete, mzee wa pindika pindua leo asema hili kesho lile,il abadirishe tabia ya ufisadi na alete maendeleo ya kweli kwa kushirikiana na hayo Dr Karume.