Mapadri Katolikiwawili wafa maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapadri Katolikiwawili wafa maji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAPADRI wawili wa Kanisa Katoliki wamekufa maji wakiogelea katika ufukwe wa Bahari ya Hindi. Mapadri hao ni Katibu wa Ubalozi wa Vatican nchini, Degn Maxime (35), raia wa Ivory Coast na John Rocksler (59), raia wa Ujerumani, aliyekuwa Mkuu wa Nyumba ya Shirika la Wabenedictin iliyoko Mivinjeni, Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, David Misime, alisema mapadri hao walikufa baada ya kuzama na kunywa maji mengi walipokuwa wakiogelea ufukweni katika hoteli ya Kasa, iliyopo Kigamboni. Misime alisema Padri Rocksler alikuwa akiishi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kurasini.
  Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10.30 jioni na kwamba, mapadri hao walifika hotelini hapo saa tano asubuhi kwa usafiri wa gari aina ya Land Rover, lenye namba za usajili T 1480 AXK. Misime alisema vifo vyao vinatokana na kushindwa kuogelea kwenye kina kirefu cha maji na kwamba, maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi. Katika tukio lingine, moto uliozuka ghafla kwenye nyumba yenye vyumba vitatu vya ofisi, umeteketeza chumba kimoja na mali iliyokuwemo ndani. Alisema mali iliyoteketea ni ya Dk. Ashock Salum na Tina Urera.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa moja usiku, eneo la Mwananyamala. Kenyela alisema chanzo cha moto huo na thamani ya mali iliyoteketea haijafahamika.
   
Loading...