Mapadri 48 wajiondoa mchakato wa kumpata Askofu Anglikana Dar es Salaam

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Zaidi ya mapadri 48 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, wameandika barua ya kujiondoa chini ya ulezi wa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledye na kudai kutoshiriki wala kujihusisha kwa namna yoyote kwenye mchakato wa kumpata askofu wa awamu ya tano wa dayosisi hiyo.

Katika barua yao ya Novemba 30 inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo wameandika namba zao za simu na kuweka sahihi, mapadri hao kutoka Nyumba ya Wahudumu wanasema wamejiondoa chini ya ulezi wa kiongozi huyo baada ya kukosa imani naye.

Kwa muda mrefu kanisa hilo limekumbwa na mgogoro wa kiuongozi, ambao ulisababisha kuondolewa kwa Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa. Katika barua yao wanasema hawatapokea huduma, maelekezo wala amri yoyote kutoka kwa kiongozi huyo na kusisitiza kutoshiriki kwa namna yoyote mchakato wa uchaguzi.

Inaendelea kuwa tayari wameandika barua mara kadhaa na kutoa tamko la kutoshiriki mchakato wa kumpata askofu mpya, wakitaka hoja zao za msingi zijibiwe lakini hawajapewa majibu. Barua hiyo inaeleza kuwa wataanza kupokea maelekezo kutoka kwa Kasisi Mkuu na kwamba, ikiwa watagundua naye anapokea maelekezo kutoka kwa askofu mkuu watafikiri vingine.

Wanasema Agosti 22 waliandika barua nyingine ikiwa na kichwa cha habari kilichoelezea ukiukwaji wa taratibu wa mchakato wa uchaguzi wa Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.

Mapadri hao kwenye barua yao, wanasema baada ya muda mrefu kupita bila majibu waliamua kukutana Novemba 17 na kuandika tamko, wakieleza kwa kina hatua walizochukua na mawazo yao kuhusu mustakabali wa dayosisi hiyo.

“Tunaamini Mungu analipenda kanisa lake la Dayosisi ya Dar es Salaam, atalilinda na kulihifadhi salama kadri ya wingi wa rehema zake,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana, katibu mkuu wa Anglikana Tanzania, Mchungaji Kanon Jonson Kinyong’ole alisema kanisa halijapokea barua hiyo na kwamba, zipo taratibu za kikatiba za vikao ambazo lazima zifuatwe wakati wa kuamua jambo lolote.

“Tunapokea barua iliyopitishwa kikatiba chini ya halmashauri, barua hiyo hatujaipata. Katiba yetu inatambua uwapo wa nyumba za Mungu na huwa zinatambuliwa wakati wa sinodi. Kwa hiyo barua hiyo sisi hatujaipokea,” alisema.

Naye askofu wa zamani wa dayosisi hiyo, Dk Mokiwa alisema hajui chochote kinachoendelea na kwamba hajaona barua yoyote iliyosainiwa na mapadri hao.

“Nipo kwenye kifungo kisicho kifungo kwa hiyo sifahamu chochote kinachoendelea. Kama nyie mna huo waraka, basi mimi haujanifikia,” alisema.



mwananchi
 
Angelikana imeanza kuwa na Mapadri lini?

Haho mapadre wa anglikana hawajaowa?
 
Angelikana imeanza kuwa na Mapadri lini?

Haho mapadre wa anglikana hawajaowa?
Anglikana Ian mapadri na ma sister na watawa wa kiume kama Roman Catholic tofauti mapadri wao wana oa. Wanaita hivyo hivyo mapadri. Was walivyo protest kutoka Roman Catholic hawakubafili chochote zaidi ya padri kuoa tu
 
Zaidi ya mapadri 48 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, wameandika barua ya kujiondoa chini ya ulezi wa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledye na kudai kutoshiriki wala kujihusisha kwa namna yoyote kwenye mchakato wa kumpata askofu wa awamu ya tano wa dayosisi hiyo

Wanaunga mkono juhudi za askofu wa awamu ya NNE hawa.
 
Back
Top Bottom