Mapacha Watenganishwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapacha Watenganishwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eRRy, Nov 17, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Kabla Ya Upasuaji​

  [​IMG]
  Baada Ya Upasuaji

  Wasichana hao wenye umri wa karibu miaka mitatu walikuwa wameungana kichwani na walikuwa wakitumia ubongo mmoja.

  Trishna na Krishna walizaliwa Bangladesh na baadaye mama yao aliwakabidhi katika kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho Australian Charity ambacho kiliwapeleka mjini Melbourne kwa upasuaji.

  Ilichukua miaka miwili kwa madaktari kufanya maandalizi ya kufanikisha upasuaji huo.

  Madaktari na manesi 16 wamefanya kazi hiyo kwa kubadilishana usiku mzima ili kufanikisha upasuaji huo.
  Leo Donnan, mkuu wa timu ya upasuaji kutoka Royal Children's Hospital, amesema “ilikuwa kama maajabu baada ya mapacha hao kutenganishwa”.

  Aliongeza kuwa: “Bado watoto hao wana wakati mgumu katika maisha yao yajayo kutokana na upasuaji huo kwani bado watakuwa na matatizo kadhaa watakayokumbana nayo baada ya upasuaji huo.”

  Kwa hospitali hiyo, tukio hilo ni la kihistoria na kwa watoto wenyewe tukio hilo ni la kihistoria zaidi.
  Hata hivyo, madaktari hao wameeleza kwamba kuna uwezekano wa mtoto mmoja au wote wawili kupata matatizo ya ubongo kutokana na upasuaji huo.

  Wahudumu wa kituo cha kulelea watoto kilichowaleta Krishna na Trishna hospitali hapo wamefurahi kupita kiasi baada ya upasuaji huo.

  “Suala hili tunaenda nalo taratibu, hatuna papara; ila kwa kweli ni hatua kubwa tuliyofikia,” alisema Margaret Smith.

  Moira Kelly ambaye ni mkuu wa kituo hicho kwa sasa ndiye mlezi wa watoto hao na kabla ya upasuaji huo aliwabusu watoto hao na kwa sasa amesema anashangazwa na jinsi hali yao inavyoendelea vizuri.

   
Loading...