Mapacha wa ajabu India | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapacha wa ajabu India

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JS, Oct 29, 2009.

 1. JS

  JS JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [​IMG] Mapacha wa nchini India, Ganga na Jamuna Mondal wenye umri wa miaka 39 maarufu duniani kama "Spider Sisters" wameungana katika namna ambayo ni nadra sana kutokea duniani kwani wameungana kuanzia kiunoni lakini kila mmoja ana mguu wake mmoja huku miguu yao ya pili imeungana pamoja na kufanya mguu mmoja wa tatu wenye vidole tisa.

  [​IMG] Mapacha hao ambao kwa siku za hivi karibuni wamejipatia umaarufu duniani kwa kucheza sarakasi kiasi cha kufananishwa na Buibui, wamekataa ushauri wa daktari mmoja wa Marekani anayetaka kuwatenganisha ili kila mmoja ajitegemee.

  [​IMG] Awali madaktari walionya kuwa kujaribu kuwatenganisha kutahatarisha maisha yao lakini daktari mtaalamu wa mapacha walioungana wa nchini Marekani, Dr James Stein aliwafanyia uchunguzi mapacha hao na amedai kuwa mapacha hao wanaweza kutenganishwa bila kuhatarisha maisha yao.

  [​IMG] "Tutaishi kama jinsi ambavyo Mungu ametuumba". Walikaririwa mapacha hao wakati wakipinga wazo la daktari James Stein juu ya kuwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha. Mapacha hao toka kijiji kimoja kidogo cha mji wa Bengal, wamekuwa wakiwavutia watu wengi kwa sarakasi zao na kupanda kuta kama bui bui, na wamekuwa wakijiingizia pesa nyingi kutoka kwa watu wanaoenda kuwashangaa. Pesa wanazozipata hutosha kuilisha familia yao kubwa yenye jumla ya watu 22 .  [​IMG] Katika kipindi kimoja mashuhuri kilichokuwa kikielezea uhalisia wa maisha yao kiitwacho "My Shocking Story: Human Spider Sisters" kinachorushwa na televisheni moja, mapacha hao walieleza kuwa watu huwashangaa wakidhani ni viumbe wa ajabu lakini wao wanajiona kama binadamu wa kawaida kwani wana sifa zote za kibinadamu.

  "Kama mlivyo nyinyi na sisi ni binadamu
  na tuna hisia kama zenu", aliongeza Jammu.  kwa habari zaidi mapacha hao waliolewa walivyokua na miaka 22 wakazaa mtoto kwa njia ya operesheni lakini dakika chahce baadaye mtoto huyo alifariki.​  Mungu na mitihani yake ya maisha wadau.  Habari kwa hisani ya Michuzi blog.
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mh! sasa kama waliolewa wana do kivipi wakati wameungana kuanzia kiunoni? je zile nanihii ni moja au mbili?nisaidieni kuelewa!
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yani hapo na mimi ndo nilishindwa kuelewa. tena waliolewa na mwanaume mmoja na ndo aliyewapa mimba. am trying to think/imagine of the process ya kumake babies with two faces looking at him sipati jibu....
   
Loading...