Elections 2015 Maono kabla na baada ya uchaguzi 2015(acording to apostle Mtalemwa Dionis)

King snr

JF-Expert Member
May 25, 2015
1,165
1,461
HAYA NDIYO MAONO NILIYOYAONA KWA NCHI YETU TANZANIA KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI. Naliona bendera ya Taifa letu ikiungua na kutoa majivu kisha nikaona zaidi haya. Najua wengine watadhihaki na wengine watatilia maanani. (1)Naliona kiongozi mkubwa wa siasa mwenye mvuto mkubwa nchini akifariki Dunia siku chache kabla ya uchaguzi na kuzuka taflani kubwa nchini.Hii itagusa nchi nzima kuliko vifo vilivyotangulia. Ni kiongozi wa juu wa chama chake,hupenda k ila kutoa maandiko mengi ya biblia akiwa kwenye majukwaa ya siasa(sijaruhisiwa kumtaja jina) nimeambiwa nimweleze na kumwombea na ntafanya hivo. (2)Vifo sasa vitahamia kwa wanachama na washabiki wa vyama vya siasa,shetani atawaingia wengi nao watachukiana na kuuwana hovyo kila kona. Si mpango wa mtu bali ni mpango wa shetani na wajumbe wake roho wachafu. (3)Kutakuwa na uadui mkubwa wa watu na vyombo vya dola kiasi watu wengi hasa vijana hawatawaamini askari polisi na hivo wataamua kufanya majukumu ambayo yangefanywa na polisi na hivyo kuleta mgongano mkubwa,muda mfupi kabla ya kupiga kura na siku ya kupiga kura wataanza kutilia mashaka magari na nyumba za kulala wageni na nyumba za watu binafsi,watakagua bila kushirikisha polisi kwa madai ya kufichua njama za kuiba kura.Polisi wakiingilia patakuwa na mgongano mkubwa. (4)Naliona kundi fulani likigomea kukubali matokeo ya Uraisi na hii italete shida sana nchini na hata wengine kuwa tayari kufa kwa ajili ya kutetea kile wanachokiita haki. Waliokataa matokeo walisema hata kama hatutawali basi tuunde serikali ya umoja wa kitaifa. (5)Kwa mara ya kwanza naliona vyombo vikubwa Duniani vikitangaza kwamba Tanzania si kisiwa tena cha amani bali ni mojawapo ya nchi ya machafuko makubwa. Nimeoneshwa hayo mara kwa mara na roho yangu imekuwa ikifadhaika sana kwa ajili ya nchi yangu Tanzania niipendayo sana.Nilikuwa siwezi yasema kwakuwa muda wa kuyasema ulikuwa haujafika. Sasa nawasihi watanzania wenzangu tumwombe Mungu na kuomba rehema. (2Nyakati 7 : 14). Ahadi ya Mungu ni kwamba tukimuomba kwa dhati. (a)Atatuma malaika wake kusimamia mchakato wa uchaguzi na kuleta usawa. (b)Atawaadhibu yeye mwenyewe wale wote wenye nia mbaya na kuiharibu nchi. (c)Atatupatia viongozi wanaostahili. (d)Atailinda nchi na kuifunika kwa mbawa za amani. *Unapoomba rehema ungama kwa ajili ya viongozi/wagombea wote wanaoenda kwa waganga na wachawi maana shetani hutumia mwanya huo kutaka kafara na damu za watu. *Ingia katika maombi ya kufunga kuanzia sasa mpaka uchaguzi hasa tarehe 20 hadi 29 baada ya uchaguzi. *Sina chama nachoshabikia bali namwombea kila mtanzania bila kujali itikadi yake.Ili uweze kuomba ipasavyo weka uvyama pembeni tuombe kwa mwelekeo wa utaifa na wala si uvyama. *Sijayaandika haya kuwatisha watu bali nimesema niliyooneshwa ili wacha Mungu wameombe Mungu atuepushe na majanga hayo. Je,uko tayari kufunga na kuomba Mungu atuepushe na haya yasitokee kwa nchi yetu Tanzania? Apostle Mtalemwa Dionis 17th October 2015.
 
Mmh nyakati za mwisho hizi tuwe macho na aina mbalimbali za unabii maana Mungu wetu ni Mungu wa haki kama haki ikitendeka naamini tutavuka uchaguzi salama lkn kukiwa na dhuluma na uonevu wowote tusitarajie muujiza.
 
Duh halikutokea hata moja yani hii tunaita mkeka umechanika baada ya kuumpa arsenal ashinde anfield
 
Back
Top Bottom