Kaisari
JF-Expert Member
- Nov 13, 2012
- 3,636
- 3,046
Nadhani,
Hapana haja ya kuitisha uchaguzi tena.
Nimeshuhudia chaguzi nyingi sana zimekuwa na misuguano mikali na hata kupoteza uhai wa watu,
Kwa machungu makubwa na kuacha baadhi ya familia na machungu makubwa.
Watu wanapigwa mabomu, wanauawa, mikutano inakuwa na kero nyingi sana na kupelekena polisi nk.
Hivi mnaitisha uchaguzi wa nini. Wakati mnataka mtu fulani ashinde. Sasa si mumteue tuu itoshe mtutangazie basi na sisi tutaridhika tuu, kama mnavyoteua mkuu wa wilaya. Basi tunaridhika. Ya nini kutupotezea muda, na nguvu kujipanga foleni kutwa nzima pamoja na muda wote wa maandalizi kumbe mnae mtu wenu mmeelekezwa ashinde. Hapana haja kutusumbua.
Hata hivyo huyo tunae mchagua halafu miezi miwili anatangaza kujiuzuru tena uchaguzi unarudiwa ya nini sasa. Maana kura zetu haziheshimiwi. Tunamfurahisha nani sasa, kuua watu, kupiga watu, kufunga watu, kwa nini. Itoshe tuu turidhike kwamba mkae madarakani mpaka siku mtakapo amua basi na sisi tunaridhika hivyo.
Hamna haja ya kuuana, kufungana, kuacha watu yatima.
Na kukejeli huku mitandaoni mnawaongezea machungu watu wenye majonzi.
Kule Arusha kuna watu walichinjwa na misumeno ya mbao, kuna mtu aliitwa mawazo aliuawa, msururu ni mrefu sana wa watu waliouawa. Sababu ni siasa, ya nini sasa hii siasa , na bado kuna watu wanakejeli sana wakiongeza machungu kwa wenzao.
Una mpiga mtu msumari wa kichwani nchi sita alafu unamuuliza unajisikiaje. !!!!!!!!!
Maoni yangu. Hizi siasa tuseme imetosha.