Maoni yangu kuhusu wagombea binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni yangu kuhusu wagombea binafsi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, May 20, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF binafsi sija wahi kuchangia kwenye swala la mgombea binafsi. Kwa sababu tunaelekea uchaguzi mkuu nimeona huu ni muda mwafaka kwangu kutoa maoni yangu kuhusu hili swala. Naomba wana JF watambue kuwa haya ni maoni yangu binafsi na wala sipo upande wa kundi lolote. Nipo tayari kusimamia hoja zangu lakini pia kusikia maoni ya wengine.

  Kwa upande mmoja naona swala la mgombea binafsi lina faa na kwa upande mwingine haufai. Nita angalia Bunge na Uraisi ambazo ndiyo taasisi kuu mbili kati ya tatu kwenye uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mgombea binafsi kwenye ubunge:
  Hapa ndipo nafikiri swala la mgombea binafsi lita kuwa na mafanikio zaidi. Mtu asiye fungana au kuji tambulisha na chama chochote anapo amua kugombea ubunge wa jimbo fulani. Kwanza ita encourage watu wengi zaidi waji husishe na siasa kwa maana mtu ahto hitaji kupitishwa na chama chake ili kugombea. Anacho takiwa ni kutimiza tu sifa na vigezo vya kuwezo kuwa mbunge na ana pewa ruhusa ya kugombea na tume. LAKINI kuna matatizo ambayo yata jitokeza hapa.
  1)Mtu kuwa mgombea binafsi ina maana itabidi awe na rasilimali binafsi kwa sababu hata kuwa na msaada wowote toka chama chochote. Fedha zinabidi zitoke mfukoni mwake au kutoka kwa wafadhili. Kwa ninavyo ona nafsi ya kupewa fedha na wafadhili itakua ndogo mno. Hata kuwa na fahari ya kuwa na vigogo wa kisiasa kuja kumpa tafu. Kwa hiyo ni watu wenye uwezo wa kipesa ndiyo haswa wata kuwa na fursa ya kutumia nafasi hiyo.
  2)Wagombea binafsi wana weza kutumiwa na vyama mbali mbali kwa manufaa yao. kwa mfano, Chama X kinaona haki kubaliki sehemu fulani basi kina amua kumsupport mgombea "binafsi". Ila huyu mgombea hata kuwa mgombea binafsi bali mtu anaye fungana na chama X kisiri siri. Huko kuta kuwa kudanganya wananchi.

  Mgombea binafsi wa uraisi:
  Kwanza hapa naona nafasi ya mgombea binafsi kushinda uraisi wa nchi bila chama ni mgumu sana. Hata "demokrasia" zilizo endelea nizi juazo mimi hawaja wahi kupata mkuu wa nchi ambae alikua mgombea binafsi(kama mifano ipo naomba). Kidogo mgombea binafsi wa ubunge anayo nafasi ya kushinda jimbo kuliko mgombea binafsi kushinda uraisi wa nchi. Kwa maana hiyo mgombea binafsi kwenye uraisi hatoa mbadala wowote.
  Tuki chukulia mfano wa endapo mgombea binafsi akashinda(bado nasimamia maneno yangu kuwa naasi ni ndogo sana) bado ata hitaji kuji husisha zaidi na chama fulani Bungeni na hicho chama kita kuwa ndicho chenye majority kwa vile ata hitaji wabunge wake kupitisha sheria mbali mbali. Kwa hiyo ita bidi afanye kwa kiasi kikubwa matakwa ya chama hicho kwa sababu yeye ata wahitaji wao kuliko wao ambavyo wata muhitaji yeye.

  Wakuu hayo ni maoni yangu tu na yanaendana na hali ilivyo kwa sasa. Mazingira yaweza badirika na wagombea binafsi wakawa na nafasi zaidi ya kuleta mabadiliko badala ya kuwa bidhaa tu ya demokrasia. Hayo ndiyo maoni yangu.
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Seconded
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hakuna lisilo wezekana..............lets get it.............

  hata kwenye vyama vya siasa vilivyopo kuna watu safi kabisa lakin wanaingia kwenye vyama hivyo bila mapenzi ya dhati.....because they have no choice.........huko nako ni kuwadanganya wananchi...............

  Kuwachagulia wananchi mtu/watu wasiowataka.............na kuwalaghai kuwa wawachague kwa vile ni wa chama fulani........ni kuwahadaa wananchi.................

  It is obvious kwamba Mgombea binafsi anaweza kuwa supported na chama fulani, watu wa chama fulani au na watu wasio na chama............sioni ubaya wake.....thats democracy

  chama cha siasa kisinizuie maamuzi ya fikra zangu............kuhusu hatima ya maendeleo ya nchi yangu..............

  ............otherwise maoni yako ni mazuri
   
Loading...