Maoni yangu kuhusu time travel kama suluhisho la kifo

JM3

Senior Member
Dec 13, 2019
158
500
Baada ya kusoma uzi wa ~Da'vinci kuhusu time travel, na kusoma maoni mengi ya wachangiaji wa mada hii inaonekana wengi wetu upeo wetu wa kufikiri ni mdogo mno, kwanza nami nianze kwa kupinga kuwa hii kitu haiwezekani na pia inawezekana nitaelezea hapa.

KWANINI HAIWEZEKANI
Unapo sema urudi nyuma kwa miaka 3000 unasahau kwamba hapa hatuangalii muda yaani saa, siku, wiki, mwezi, mwaka na miaka hapa tutaangalia matendo ambayo yalikwisha tendeka miaka hiyo mfano miaka 200 iliyopita siku ya jmatatu bwana davinci alikuwa anataka kumuua mkewe na kweli akamuua ( hapa ina maana mke kafa + plus kitendo tayari kimetendeka na miili ilishaoza ) ina maana hata Kama umerudi kwenye miaka hiyo huwezi zuia lile Tendo kwa kuwa lisha tendeka hivyo ni kitu ambacho hakiwezekani.

KWANINI INAWEZEKANA NA NI KWA JINSI GANI
Hapa tunaenda kiroho zaidi, ili hii kitu iwezekana ni lazima Mwili ufe ibaki nafsi yako wengi tunaamini nafsi haifi, then ile nafsi ndo ina uwezo wa kufanya mambo ya past, present na future, mfano ni pale unapo kuwa umelala ukaanza kuota Mambo ya zamani kweli yaliyo wahi kutokea na kipindi hicho wenda ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa ushazaliwa, pia una uwezo wa kuota Mambo yajayo mfano unaota umekuwa tajiri mkubwa unakula raha za kila Aina kumbe tu ni nafsi na sio Mwili na ukitaka kuamini kuwa ni nafsi ni pale unapo amka nakurudi katika Hali ya kimwili Yale uliyokuwa unayaota hutoona hata moja japo kuwa yapo mengine hutokea baadae kama ulivyo ota.

Kwa kumalizia ni kuwa Kuna maisha Baada ya kifo, nilishawahi kusoma simulizi moja ya jamaa aliyegongwa na gari Baada ya muda nafsi yake ikatoka katika Mwili na Mwili ukabaki pale alipokuwa amelala yaani alikuwa anajiona Mara mbili amelala na huku ameshaamka anajishangaa japo alicho kuwa anaongea walimwengu walikuwa hawawezi kumsikia wala kumuona na alikuwa hawezi kushika chochote cha ulimwengu na alipo kuwa akitembea hatua 1 ni sawa na Kama km 5 alikuwa na uwezo wa kukimbia na kuiacha gari mara 10 zaidi,

Nawasilisha hoja.
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,259
2,000
Hiyo idea itabaki tu kwenye vitabu na komputa zao, ni ngumu mno maana inataka sasa kupingana na nature.

Its beyond human capabilities
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom