Maoni yangu kuhusu 'Maoni ya Dr. Slaa' juu ya pesa za wahanga wa tetemeko Bukoba

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Nimesoma maelezo ya Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa juu ya hatua ya serikali kutumia fedha za misaada za wahanga wa Bukoba kutaka kujenga miundombinu ya serikali kama ofisi za idara na taasisi za serikali, mashule, barabara etc.

Dr.Slaa ameunga mkono hatua hiyo ya serikali. Katika maelezo yake aliyoyatoa kwa Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Kilimanjaro Ndg.Kibona Dickson, Dr.Slaa amejieleza kwa kirefu sana kwanini anaunga mkono hatua hiyo ya serikali ambayo wananchi wengi wameonesha kutoridhishwa nayo. Maelezo ya Dr.Slaa yana hoja mbili kubwa:

1. Hoja ya kwanza ya Dr.Slaa ni kile kinachoitwa katika ethics "Lesser evil". Yani yanapotokea makosa mawili na ukahitajika uchague moja basi unachagua lenye nafuu zaidi. Dr.Slaa anasema ni heri serikali itumie pesa hizo kuwajengea wananchi miundombinu kuliko kuwatelekeza kabisa.

Ametumia mifano miwili kutetea hoja hiyo:

Mfano wa kwanza, ni maafa yaliyotokana na mvua mkoani Shinyanga wilayani Kahama, ambapo Rais Kikwete aliwaahidi wahanga kuwajengea nyumba lakini Rais Magufuli akaja kufuta ahadi hiyo. Kwahiyo Dr.Slaa anaona kuliko serikali iwaahidi tena wananchi "ahadi hewa" ya kuwajengea, ni bora iseme ukweli kuwa itashindwa kujenga badala yake itajenga miundombinu tu.

Mfano wa pili, Dr.Slaa katumia mafuriko ya Kilosa mkoani Morogoro. Amesema wahanga wametelekezwa kwa zaidi ya miaka 10 bila msaada wowote licha ya ahadi kedekede za serikali kuwasaidia. Dr.Slaa anasema serikali iliwapa wahanga hao viwanja vya kujenga lakini vikavamiwa na viongozi wa serikali ngazi ya mkoa, wilaya na kijiji na kujigawia.

Kwa mujibu wa Slaa ni bora serikali iseme ukweli kuwa haitaweza kuwajengea wananchi kuliko kuwapa matumaini "hewa" au kuwaahidi halafu ikashindwa kutimiza. The theory of lesser evil.!

2. Pili Dr.Slaa amesema si jukumu la serikali kujenga makazi ya watu waliopata maafa, kazi ya serikali ni kujenga miundombinu tu. Na miundombinu ikijengwa itarahisisha zoezi la wananchi kujijengea makazi yao kuwa rahisi.

Dr.Slaa ametumia mfano wa jimbo moja huko Canada anapoishi kwa sasa kutetea hoja yake. Anasema nchini Canada katika Jimbo la Alberta, Mji wa McMurray, watu zaidi ya 70,000 walikumbwa na janga la moto uliokuwa unapelekwa kwa mwendo kasi mkubwa wa upepo. Watu hao waliokolewa lakini moto huo uliteketeza za nyumba zao.

Dr.Slaa anasema "Tulichangishwa kwa hiari na Red Cross, shule, Mamlaka za miji na Mitaa kwa njia mbali. Lakini, fedha zote hizo zilienda kujenga miundombinu, na huduma ya dharura ya muda mfupi kama nilivyoeleza juu. Wananchi waliopoteza nyumba zao walielekezwa kutumia " Insurance" zao" ili kufidiwa nyumba zao zilizoteketea kwa moto.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]
Napenda niseme kwa kifupi kuhusiana na tamko hili la Dr.Slaa.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG], Dr.Slaa aelewe kwamba uovu hauwezi kutumika kuhalalisha uovu. Yeye ni Mkristo na amewahi kuwa kiongozi wa dini hivyo anafahamu kuwa dhambi haiwezi kutumika kutakatisha dhambi. Kama wananchi wa Kahama na Kilosa walidhulumiwa, kutapeliwa au kupewa ahadi hewa na serikali haiwezi kuwa kigezo cha kuhalalisha wananchi wa Bukoba nao kutapeliwa.

Ningemuelewa Dr.Slaa kama angetumia mifano ya Kahama na Kilosa kuionya serikali kuwa isijaribu tena kufanya ujinga wa aina hiyo badala ya kutumia mifano hiyo kuhalalisha utapeli wa serikali. Kwa mfano Dr.Slaa angeweza kusema "Tunajua namna serikali ilivyowaahidi wahanga wa Kahama na Kilosa kisha kuwatelekeza, kwahiyo tunaitaka serikali ya Magufuli isifanye yaliyofanywa na serikali iliyopita maana wananchi hatutakua tayari"

Lakini Dr.Slaa kusema serikali ilishawahi kuwatapeli wahanga wa Kahama na Kilosa bila kuwajengea nyumba wala miundombinu, kwahiyo ni bora iwajengee hata miundombinu hawa wa Bukoba, ni kauli ya kukata tamaa.

Ni sawa na kusema unakubali mwizi aje akuibie kisa tu hajajeruhi mtu. Kwamba una historia ya kuibiwa na kujeruhiwa kwa hiyo huyu aliyekuja kukuibia tu bila kujeruhi unamuona ni wa "maana zaidi" kuliko hao waliokuibia na kukujeruhi. Hii si sahihi hata kdg. Two wrongs never make it right.!

[HASHTAG]#Pil[/HASHTAG], Dr.Slaa amesema si JUKUMU la serikali kuwajengea watu makazi. Kwamba wananchi wanapaswa kujenga makazi yao wenyewe na serikali ijenge miundombinu tu. Hoja hii ya Slaa ingekua sahihi kama serikali ingekua inatumia pesa zake yenyewe (za mfuko wa maafa) na sio pesa za wasamara wema zilizochangishwa makanisani, misikitini, makazini etc.

Dr.Slaa anajua serikali ina mfuko wa maafa. Na mfuko huu hutengewa fedha kila mwaka kwenye bajeti. Kwahiyo ni vizuri pesa za mfuko huo zingetumika kukarabati miundombinu badala ya kutumia pesa hizi za msaada ya wasamaria wema.

Pesa za msaada zilielekezwa kwa wahanga "specific" kwahiyo kupindisha matumizi yake ni "utapeli". Hata ujumbe uliokua unatolewa na serikali wakati wakiomba misaada hiyo walisema "changia WAATHIRIKA wa tetemeko Bukoba" na sio "Changia miundombinu Bukoba"

Kwahiyo misaada iliyokua ikitolewa ilielekezwa kwa waathirika na sio kujenga miundombinu. Hakuna tangazo lolote lililosema "Changia miundombinu iliyoharibika Bukoba". Hakuna. Kama serikalili ingetaka kuchangia miundombinu ingeanzisha kampeni maalum ya "Changia miundombinu" halafu ione watu wangapi wangechangia.

Lakini ujumbe ulikua "Changia waathirika Bukoba" leo pesa hizo zimepelekwa kujenga miundombinu, Je Dr.Slaa haoni huu ni utapeli? Katika kanisa nalosali tuliamua sadaka zote za jumapili moja zipelekwe Bukoba kusaidia wahanga. Sasa je, unadhani waumini wanajisikiaje kuambiwa sadaka yao waliyoitoa kwa ajili ya wajane, yatima, wazee na wahanga wengine zimepelekwa kujenga mashule na barabara? Yani watu wanajengewa shule na hawana pa kukaa.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG], Mwalimu wangu huyu wa siasa Dr.Slaa anajaribu kutumia mfano wa Canada kwa matatizo ya Tanzania anasahau kwamba hizi ni nchi mbili tofauti, zenye maendeleo tofauti, tamaduni tofauti, aina ya uongozi tofauti, na hali ya kiuchumi tofauti. Huwezi kuwaambia watanzania wajenge makazi yao wenyewe kisa huko Canada walijenga wenyewe.

Slaa anakiri kwamba Canada wananchi wengi wana bima (insurance) za nyumba zao na walipopata majanga walilipwa na makampuni hayo ya Bima. Lakini je hapa Tanzania ni watu wangapi wamekatia Bima nyumba zao? Katika majiji makubwa kama Dar, Mwanza na Arusha ni asilimia ndogo sana ya watu wenye Bima za nyumba, sembuse Bukoba?

Hata magari tu kuna watu wanakata Bima ili kuepuka usumbufu wa askari barabarani, na sio kulinda gari lake. Kwa kifupi hatuna elimu ya kutosha ya masuala ya Bima na umuhimu wake. Wengi wanaona kama ni kupoteza hela tu. Sasa Dr.Slaa anawezaje kujustify hoja yake kuhusu Bima huku akijua wazi suala la bima kwa nchi yetu ni changamoto?

Kwa kifupi niseme tu kuwa Mwalimu wangu huyu wa siasa, na kiongozi wangu wa zamani ninayemheshimu sana ameteleza kuhusu suala hili la maafa Bukoba. Amekosea na pengine atahitaji kuwaomba radhi watu wa Bukoba.

Serikali inapaswa kutoa pesa zote ilizochangisha kusaidia waathirika wa maafa ya Bukoba, na ni LAZIMA ishinikizwe pesa hizo ziwafikie walenga (Si lazima wapewe cash, maana kuna watu wanaweza kuhoji modality ya kufikisha msaada huo kwa walengwa na kuhamisha mjadala. Issue hapa sio cash. Issue ni msaada ufike kwa walengwa. Wanaweza kupewa saruji, mabati, tofali etc lakini lazima msaada huo uwafikie).

Then katika kujenga miundombinu serikali itafute njia nyingine ya kufanya, ikiwa ni pamoja na kutumia fedha zake kutoka serikalini (mathalani mfuko wa maafa), na sio hizi zilizochangwa na wasamaria wema.!
 
Slaa amesahau kuwa Watanzania hatuna bima za majanga.
Ili nyumba ikatiwe bima ni lazima iwe na hati sio offer wala Leseni ya makazi.
Kagera nyumba ngapi zina hati? Tena nyumba ni lazima ifanyiwe valuation na registered valuer . Wangapi wanamudu gharama hizo? Tuwe wakweli na wahalisia CCM ni ileile iliyowatelekeza kahama ndio CCM hii hii iliyowatelekeza wana Kagera
 
Tatzo lako wewe nae unajiona NI GWIJI zaidi ya Dr SLAA ya kwamba hoja zako ni BORA SANA KULIKO ZAKE.....kijana hauna huo usafi wa kuweza kubishana na huyo MZEE NA SI SAIZI YAKO hata kidogo na ni miongoni mwa vijana wa wanafiki wakubwa ndani ya nchi hii....

HILI SUALA LA TETEMEKO LA KAGERA kuhusu kuwejengea WAHANGA hata Dr MAGUFULI halilikataa mapema kabsa around SEPTEMBER hivi tafuta clip yake YOU TUBE...akasema SERIKALI HAITAWAJENGEA WAHANGA WA TETEMEKO bali hizo pesa zitatumika KWENYE MIUNDO MBINU....sasa nyie wapinzani UCHWARA MKAACHA KUISHIKIA KIDEDEA KAULI YA MTUKUFU RAISI....mkaja ishikia kidedea kauli ya MKUU wa mkoa maana mmeona huyo ndiyo saizi yenu.....

HALAFU NAONA CHADEMA HILI MMELISHIKIA KIDEDEA KWELI ili mpate pa kutokea..... TAFUTENI ALICHOKISEMA RAIS KUHUSU HIZI PESA MWEZI SEPTEMBER afu mrudi hapa mseme kwanini hamkupingana na hiyo kauli kipindi hicho au kwa sababu kulikuwa na UKUTA??? na sasa hivi mmeshindwa kwenye UKUTA mmelishikia kidedea hili....\

Aiseeeh huu ndio upinzani
 
Kila mtanzania ana haki ya kutoa mwelekeo wake wa maoni juu ya chochote.
sio lazima unavyoona wewe au wengi wote waone hivyo.

A: Unaweza kuwagawia Pesa na misaada yote Equally(Kuna hatari kila kaya kupata NUSU BATI, au misumari miwili miwili) au Equitably(Masikini sana wakapewa kingi na wenye nafuu wakapata vichache japo havitatosha hata kwa mwezi na hatuna mkataba na Mungu kama Hakuna janga jingine sehemu nyingine)

B: Uwawekee Miundombini ya haraka itakayowarahisishia Kupata unafuu kwa Muda mrefu Huku ukijikita kuwapa misaada direct kabisa wale wasiojiweza wazee,wajane na watoto.

A =B zote ni sawa, unategemea unaangalia kutokea angle gani.

Hayo maamuzi aliwahi kuyasemea baba wa taifa kuhusu matumizi ya misaada. Umepata msaada wa Kusaidia Familia Masikini, A Umpe pesa au Chakula ale kisha ziishe aombe tena wakati msaada ukiwa umeisha. Au B umsomeshe mtoto wake wakati yeye anajihudumia. Mtoto akifanikiwa na Elimu ikimkomboa atakomboa familia yake yote hadi kufa. Yote ni Mipango.

hapa kati yako na Dr option zote ni Sawa, Tofauti Option ipi ni sawa zaidi. Hii haimuliwi kwa kudhani bali inategemea matokeo ya Utafiti wa Janga Husika. Pesa za Majanga Ya KGR zitatue majanga ya BK huku zikisapotiwa na Emergency (Mfuko wa Majanga kiasi) maana huwezi jua nini kitatokea kesho penginepo tanzania na ukakoswa msaada na Akiba ya Majanga yote umeelekeza sehemu Moja. Hapa ni Mipango na Maamuzi
 
Hela za tetemeko ni lazima zimtokee puani mtu .
Ona sasa akili zako zilivyo kaa kushoto.....tatzo lenu mwisho wa siku mnashindwa kusimamia kauli zenu......hivi mbna hamkupiga kelele kipindi kile RAISI ANATOA TAMKO JUU YA MATUMIZI YA HIZI PESA au kwasababu kulikua na vuguvugu la UKUTA?????sasa ukuta umeshindika mnatafuta nitoke VIPI kupitia hili....
 
Bima zipo tatizo ni wewe ambaye hutaki kuziwekeza mali zako kinga ya bima
Ili nyumba ikatiwe bima ni lazima iwe na hati sio offer wala Leseni ya makazi.
Kagera nyumba ngapi zina hati? Tena nyumba ni lazima ifanyiwe valuation na registered valuer . Wangapi wanamudu gharama hizo? Tuwe wakweli na wahalisia CCM ni ileile iliyowatelekeza kahama ndio CCM hii hii iliyowatelekeza wana Kagera
 
Ona sasa akili zako zilivyo kaa kushoto.....tatzo lenu mwisho wa siku mnashindwa kusimamia kauli zenu......hivi mbna hamkupiga kelele kipindi kile RAISI ANATOA TAMKO JUU YA MATUMIZI YA HIZI PESA au kwasababu kulikua na vuguvugu la UKUTA?????sasa ukuta umeshindika mnatafuta nitoke VIPI kupitia hili....
Kuna kila dalili kwamba Hela za tetemeko zitaleta uchaguzi mpya .
 
Canada au nchi za Magharibi kila nyumba inakuwa na bima kwa ajili ya majanga. Bima hiyo ndio inagharamia ujenzi wa nyumba za watu wakati serikali ikihangaika na miundombinu.

Dr Slaa, TZ ni tofauti na Canada. KwaTZ Mhanga namba moja ni wananchi na kwasababu hawana bima yoyote, misaada lazima ianzie kwao.
 
Huwa nachoka pale mtu mwenye uelewa kama wa Slaa anapoujua ukweli lakini anaamua tu kuupindisha kwasababu anazozijua yeye mwenyewe. Sasa hivi kweli Slaa hajui kwamba Watanzania wengi hawana bima za nyumba? Alitaka kuwa Rais huyu!
...Na kuahidi, akichaguliwa kuwa Raisi, angewezesha BEI ya SARUJI kuwa Shilingi 5000 Nchi nzima. Kutokea Wazo Hill hadi Manyovu, Namanga hadi Rusumo, Holoholo hadi Momba, Itigi hadi Matai....Butiama hadi Nangulukulu..Ukara hadi Kilindoni. Mutukula hadi Nanyumbu. Hanga hadi Msalala. Kikatiti hadi Mkalama. Mulbadaw hadi Kingosera. Nchi NZIMA.....
 
Back
Top Bottom