Maoni yangu: Biashara za simu used na wizi wa simu

Maoni yangu: Biashara za simu used na wizi wa simu

h120

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
2,545
Reaction score
3,370
Salaam,

Kama kichwa cha mada kinavyotambulisha nataka kuzungumzia changamoto ya biashara za simu used.

Tunajua upatikanaji wa simu used (zilizotumika) ulivyo.

1. Unaweza ukawa ulinunua simu mpya umeitumia miaka au miezi au siku kadhaa kwasababu mbalimbali ukaamua kuiuza, hii haitatambulika tena kama ni simu mpya (Brand new) hata kama uliitumia siku mbili tu tangu uinunue.

2. Wizi simu inaibiwa katika tukio la kihalifu linaloweza kuhusishwa na vifo majeraha na uharibifu wa mali, simu inapopatikana mazingira haya inapelekwa sokoni na kuuzwa.

Baada ya kuuzwa kinachofuata, kwa aliyeibiwa ataenda polisi kutoa taarifa kitengo cha cybercrime na atafuata taratibu zinazohitajika kisha wanausalama kwa kushirikiana na mitandao ya simu huanza kufuatilia simu ile.

Umenunua simu kwa pesa ulizovuja jasho unakuja kukamatwa kwa kuhusishwa na uhalifu hapo nadhani mnajua dhahma itakayomkumba aliyekamatwa na simu. kama huna pesa basi chamoto utakipata kama zipo basi mtajuana na mamwela na aliyeibiwa.

Ukifatilia nilichoandika hapo juu, utaona kila mtu ataingia uwoga wa kununua simu zilizotumika kwa kuepusha matatizo ya kubambikiwa au kuhusishwa na kesi za jinai endapo simu iliyonunuliwa ilipatikana katika mazingira hayo.

Kuepukana na hizo changamoto watu wengine wamekoma kabisa kununua simu used na hawataki kusikia, wengine wanataka wahakikishiwe na muuzaji uhalali wa umiliki wa simu husika hivyo hudai risiti au kwenda kuandikishana endapo kutatokea jambo lolote iwe rahisi kuchukuliwa hatua anaye husika.

Inapotokea umepoteza risiti au huna kabisa tayari unakosa fursa ya kuuza simu yako kwa baadhi ya watu, kwa kuhofia tu simu za wizi.

HAYA NI MAONI YANGU KUHUSU KUPUNGUZA CHANGAMOTO KWA WAUZAJI NA WANUNUZI WA SIMU USED

TCRA kwa kushirikiana na jeshi la polisi waunde mfumo wa portal.

Hii portal itafanya nini?
Hii portal itatumiwa na jeshi la polisi kitengo cha cyber crime kufanya blacklist ya simu zote zilizoibiwa ama kupotea kwa mfumo uleule wa IMEI number. hilo litafanyika baada ya mpeleka malalamiko kutimiza taratibu zote za loss report.

Nini tofauti ya portal na mfumo unaotumika sasa?
Portal itamruhusu mtu yeyote kuangalia simu anayotaka kununua kama haipo kwenye blacklist, kwa maana kama nataka kununua simu fulani nitamwambia muuzaji ni lazima nijihakikishie hii simu unayoniuzia haijawa reported kama imeibiwa au imepotea, baada ya hapo basi mteja atakua na uhakika wa anachokinunua.

Faida ya Kuingiza mapato?
Mfumo wa portal utaliingizia mapato aidha jeshi la polisi au TCRA kulingana na atakae endesha huo mfumo, kuangalia simu kama haijaripotiwa sio bure lazima ulipie kwa mitandao ya simu ndipo uweze kuangalia, wanaweza wakaweka kiwango cha 1000 mpaka 5000 hizi ingawa 2000 ingetosha. kwa hiyo kila unapotaka kuangalia simu unayotaka kununua kama ipo clean unalipia 2000.

Sifa za ziada
Kwa kuwa huu mfumo lengo kuu ni kupunguza matukio ya wizi wa simu kuna sifa za ziada zitakwepo ili kufanikisha kuwakama au kuwafatilia wahalifu au wezi wa simu.

Sifa ya kiusalama ya huu mfumo ni hii hapa kabla sijaielezea kumbuka ni vizuri muuzaji afanye zoezi la kukuhakikishia kwamba simu anayouza ni halali hivyo mnaweza changana kulipia ila sharti hili zoezi la uhakiki lifanyike kwenye kifaa au simu ya muuzaji.

Hii sifa ya ziada ni uwezo wa portal kuchukua taarifa ya simu iliyotumika kuhakiki uhalali wa simu nyingine endapo IMEI number iliyoangaliwa imeonekana kwamba imeripotiwa, kwa hiyo taarifa zitarudi kule kwa waongoza mfumo kuwapa leads za kwamba simu fulani imetumika kuangalia nambari ya IMEI iliyoripotiwa kuibiwa hivyo kuwapa urahisi wana usalama kufatilia yule muuzaji na chain yake yote.

Haya IT na Computer science eng wazo hilo la bure kabisa tengenezeni mfumo mkale pesa za TCRA na polisi.

NB: Najua kuna wale wa kubadilisha IMEI ingawa ni kinyume cha sheria.

Mfumo ukitengenezwa commision yangu tafadhali hata credit tu kama wazo litatoka humu.
 
Back
Top Bottom