Maoni yako yapo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya?

Maoni yako yapo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya?

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Tayari malalamiko yameshaanza kutolewa kwa watu mbalimbali kuhusu maoni yao kutoingizwa kwenye Rasimu ya Katiba Mpya. Hivyo basi, EMT na timu yake wameamua kufanya review ya maoni yaliyotolewa na Wana-ChitChat ili kujua kama yameingizwa kwenye Rasimu ya Katiba Mpya. Tafadhali weka maoni yako hapa, ambayo yametupwa kapuni.

Katika maoni yangu niliyoyatoa kwenye Tume ya Katiba nilighusia zaidi matumizi ya lugha hasa kwa vijana wa teke linalokujia na kushauri kuwa kuna umuhimu wa kuwepo kipengele kwenye Katiba mpya ambacho kitataka taasisi mbalimbali kusimplfy lugha wanayotumia kwenye maandishi ili iendane na lugha ya vijana. Hii itawafanya mayanki kuwa interested kusoma na kufuata maandishi na matamko ya hizo taasisi.

Hata hivyo, nimeshangaa sana hakuna kipengele kama hicho kwenye Rasimu, japokuwa wajumbe wengi wa Tume ya Katiba Mpya walionyesha kuniunga mkono moja kwa moja. Kwa mfano, nilitoa maoni yangu kuwa, ili vijana wasome zaidi vitabu vya dini, inabidi vinaandikwe "kiaina". Kwa mfano, nilishauri sala ya Baba Yetu iandikwe kwa lugha ya "masela" ili iflow kama ifuatavyo:

"Niaje Dingi letu uliye majuu, jina lako lipewe maflag ya kufa mtu, ufalme wako utuibukie kiana,
Unachotaka kifanyike duniani kiwe mzuka kama maskani kwako,

Utuletee leo msosi wa kumwaga, mabaga na mazagazaga kibao,
Tuchukulie poa kama tukichemka kama nasi tunavyopotezea waduanzi wetu,

Usitubwage kiaina katika zali bali utusepeshe fasta kwa yule mwanaharam,
Kwa kuwa uko juu kinoma, una mapower na maujanja ya kumwaga.

AMINA."
 
Achana na kuchezea hili sala,
kivyangu nakuona kama kilaza.
 
Back
Top Bottom