Maoni Yako Rasimu ya PILI ya KATIBA,Kipi kitoke na kipi kibaki?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
2,000
wadau
tumeipata Rasimu ya PILI ya katiba yetu ya Tanzania na kama alivyosema Mh Rais mitandao ya kijamii kama JF inaweza kutumika kukusanya maoni na kuwasaidia wale watakaopata nafasi ya kutuwakilisha ktk bunge la KATIBA mwezi wa pili kuwa na pakuanzia.
Tunaweza kuanzia hapa ktk kutoa maoni yetu,kipi kitoke,kipi kibadirishwe na kipi kibaki na kwanini.

kwa uapnde wangu nimefurahi sana kuona uwepo wa uraia pacha na ningeomba watakaopata nafasi ya kutuwakilisha ktk bunge la katiba waendelee kulikubali hili,ili tuweze kuwarudisha watanzania waliopo nje na kuwa raia wa nchi hizo kuja kuwekeza Tanzania ikiwa kama ni nchi yao ya kuzaliwa bila vikwazo vyovyote vile.
yapo mengi ya kusema,ila ningeomba nianze na hili la uraia pacha.
karibuni wadau,tuache kushindana,kwani hatapatikana mshindi ktk hili na mwisho wa siku itakayo umia ni nchi na watu wake ambao ni sisi.
TUENDELEE KUTOA MAONI YETU NI MUHIMU KWA TAIFA LETU
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom