Maoni yako kwa katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni yako kwa katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by KakaKiiza, Jan 6, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,268
  Trophy Points: 280
  Nini maoni yako kwa katiba mpya?
  Rais apunguziwe nini??
  Tume ya uchaguzi iweje?
  Mawaziri wateuliwe nani?
  Mikataba yote ipitiwe na bunge?
  Rais ashitakiwe pale anapofanya makosa?
  Je Rais apigiwe kura yakutokuwa na imani?
  Endelezeni.............
   
 2. K

  Kwiifoenda Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaji mkuu ateuliwe na nani? DC, DAS na RAS waondolewe? Wanaotajwa kwenye kashfa mbalimbali wazuiwe kugombea nafasi yeyote mpaka wasafishwe na mahakama? Waziri mkuu ateuliwe na nani? Mtu akichaguliwa kuwa rais aachie uenyekiti wa chama cha siasa?
   
 3. T

  Tunsume Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Mjadala wa aina gani ya katiba inaifaa Tanzania, ni vizuri uanzie kwenye mambo ya msingi ambayo tunataka katiba mpya iyarekebishe na kuyajenga. Tanzania inahitaji Katiba endelevu na si dumavu kama hii tuliyonayo sasa. Msingi mkuu wa mazungumzo katika katiba mpya ni swala la Uhuru wa wananchi/jamii (individual freedoms) na kiasi gani cha uhuru huo ubaki kwa wananchi na kiasi gani kiende kwa dola/watawala. Kwa maoni yangu, katika katiba mpya, uhuru mwingi uwachwe kwa jamii na tuweke kiasi tu kwa dola. Pia hata hicho kiasi tutakachoacha kwa dola lazima tushirikishwe kama jamii/wananchi katika kuutekeleza/kuutumia uhuru huo. Kwa maana hiyo, Judge Mkuu anaweza kuteuliwa na Rais lakini lazima apitishwe na Bunge na Wananchi. Kwa maana kwamba, wale wenye sifa za kuwa majudge wakuu wataomba, jamii itapewa nafasi kuwachunguza na kutoa taarifa za kufaa ama kutofaa kwao; baada ya hapo Rais atapendekeza jina na kupeleka kwa bunge. Vigezo vya sifa na stahili ya kuwa mtumishi wa umma ndiyo vitatumika kumchagua Judge Mkuu. Vigezo hivi lazima vifanywe mojawapo ya sheria inayoidhinishwa na Katiba Mpya. Vigezo hivyo vitawabana wote wanaoteuliwa kushika nyadhifa zozote kwenye utumishi wa umma (siasa, serikali hata asasi zisizo za kiserikali lakini zenye dhamana ya kutumikia umma).

  Majudge wengine watapitishwa na Judicial Service Commission na wajumbe wake pia watateuliwa na Rais na kupitishwa na Bunge. Nao pia watatakiwa wapitie utaratibu wa kuchunguzwa na wananchi na wanaofaa kukubalika wapitishwe na Bunge. Tukifuata mtindo huu ina maana wananchi watashiriki kutekeleza uhuru waliokabidhi dola. Katika mfumo huu itakuwa ngumu sana kwa Rais kuteuwa mtu anayempenda tuu kwasababu ama amependekezwa na awapendao au anauwezo mkubwa wa kulinda maslahi yake.

  Kuhusu nani atachagua Ma DC, labda swala la awali lingeanza kuwa jee ni muuondo gani wa serikali tunaotaka, kwanini na unatatua matatizo gani ya kiutawala yanayoletwa na Katiba ya sasa. Sifa nyingine ya Katiba endelevu ni kusogeza mamlaka na utawala kwa jamii na kuhakikisha jamii inajiamulia mambo yake yenyewe. Pili, katiba endelevu huweka mfumo unaorahisha upatikanaji huduma kwa wananchi. Kama nia yetu ni kupata katiba endelevu, ni lazima tuwe na mfumo wa mikoa ama majimbo yenye mifumo ya kufanya maamuzi yake na kujiendesha kiutawala. Tanzania ni kubwa sana kutawaliwa kutoka Dar es Salaam. Ma DC wanaweza kuendelea kuwepo kama wawakilishi wa serikal ya Kitaifa na siyo serikali kuu, lakini uteuzi wao utafuata mtindo ulel ule kama tuliouweka wa majudge. Ikumbukwe Ma-DC kama watabaki watawajibika kiutawala kwa serikali ya kitaifa. Katiba Katiba endelevu hatuna serikali kuu kwasbabu mamlaka yanakuwa yamesambazwa kikamilifu kwa wananchi. Aina ya ugatuzi tunaokuwa nao ni ile ya majimbo/mikoa inayojitegenea na mabunge yake, budget zao na maamuzi yao mradi yanazingatia miongozo ya kitaifa.

  Katiba endelevu inakuwa na miiko na maadili ya uongozi ambayo yako moja kwa moja na yanatekelezwa kupitia sheria ya sifa/wasifu wa watumishi wa umma na watoa huduma kwa umma. Inawabana wote wanaohusika na utoaji huduma ikijumlisha makontrakta binafsi, watumishi na wenye asasi binafsi ikijumlisha vyombo vya kidini. Kwa maana hiyo yeyote aliyehusika na rushwa, ama matendo yeyote kinyume na misingi iliyokubalika na jamii kupitia katiba, hatastahili kuwa kwenye uongozi na utumishi wa umma. Hivyo kama mtu aliiba kwenye asasi isiyo ya kiseriali, ama kanisa ama utumishi wa umma hata faa kwa nyadhifa yeyote kwa maana ya katiba endelevu.

  Swala la Mawaziri wateuliwe na nani- nalo liangaliwe kwa mapana ya kwamba tunataka kutatua matatizo gani yanayorudisha ustawi/maendeleo ya wananchi/jamii katika katiba ya sasa. Tumeona kuwa, uwajibikaji wa viongozi/watatwala kwa maendeleo/ustawi wa jamii umekuwa hakuna ama mdogo kwasababu mawaziri wanawajibika zaidi na kujali zaidi ustawi wa waliowateua. Hivyo basi katika hali hiyo tuwe na mfumo utakaoondoa madaraka makubwa ya watatwala kuteuwa watendaji wakuu wa kisiasa na kiutawala. Pia tumeona kuwa mfumo tulionao ni mbovu katika uwajibikaji kwasababu unaruhusu muingiliano wa kiutendaji na kimamlaka kati ya mihimili 3 ya dola yaani, bunge, sheria na serikali. Hii imekuwa sababu kubwa ya mihimili ypote mitatu kutokuwa na uwajibikaji. Kitendo cha kuteua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge kinapunguza uwajibikaji wao (ambo ni sehemu ya utawala/executive/utendaji) Hivyo basi tungefikiria mfumo ambao mawaziri hawatoki sehemu ya bunge na ni watu tofauti wanaomba kazi, kuchunguzwa na wananchi, kuteuliwa na rais na pupitishwa na bunge.
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwiifoenda; shiifonisha mbee

  ibadilishwe tu akuna kuweka viraka
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,268
  Trophy Points: 280
  Vilaka nivitu vilivyopitwa na wakati na kuenzi mawazo ya mkoloni!!
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Napendelea iwepo katiba mpya.

  Kifungu cha Rais kuwa maximum kuchaguliwa mara mbili kiondolewe. Maximum ya kuchaguliwa Rais ni pale atapoamuwa mwenyewe kuwa sasa basi au atapokosa kuchaguliwa.

  Ikipita hiyo ntafurahi sana, ningependa Kikwete aendelee kuwa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha pili.
   
Loading...