Maoni ya wanasheria kuhusu tukio la Makonda

Maoni ya wanasheria kuhusu tukio la Makonda

Naona Tundu Lissu na wenzake wana wadanganya...! Matusi ya kubenea yalikuwa yanataka kuhatarisha amani na kuleta vurugu hivyo Paul Makonda alitumia busara ya hali ya juu kumuweka ndani(kumpumzisha) hata Lissu akileta ngebe atapumzishwa..!

Kubenea anapaswa kufunzwa jinsi ya kufanya kazi na serikali na kujua mipaka yake....
Tundu Lissu alichosema ni hoja za kisheria zinabaki kama zilivyo kama una hoja kinzani iweke tuone sio unasema kadanganya ww wa wapi!?
 
Last edited by a moderator:
Mbona hawajaongelewa matusi ya mwenzao?!! Je? Ni halali kumuita mwenzio kibaka???

Hivi kibaka ni nani ili tuone kama ni tusi au kama alichokifanya Makonda kinastahili kuitwa kibaka? Najiuliza pia mfano kuna wale wanaosema "kibaka wa demokrasia", "kibaka wa uhuru wa vyombo vya habari" etc.
 
Mliambiwa katiba ni ya 1977.tujadili rasimu mkaweka mpira kwapani kwa kutoka nje ya bunge .mtoto ukawa akazaliwa.kufuta kipengele ndani ya katiba siyo jambo rahisi kihivyo rejea mgombea binafsi kuna ruling ya mahakama ipo.cha msingi hapa ni viongozi waheshimiane na wajue mipaka yao na protokali.viongozi wageni ktk tasnia ya utawala wajifunze.hivi mh.mbunge nasari ni kijana mdogo anayoyafanya kwa wapiga kura wake awe role mode wao au mh.mdee mh.sakaya mh.kihwelu wajifunze kwao siyo kutunishiana misuli
 
Hivi kibaka ni nani ili tuone kama ni tusi au kama alichokifanya Makonda kinastahili kuitwa kibaka? Najiuliza pia mfano kuna wale wanaosema "kibaka wa demokrasia", "kibaka wa uhuru wa vyombo vya habari" etc.

mtu akifikishwa mahakamani kwa kosa la kubaka na akakutwa na hatia si anakuwa kibaka. Sasa kubenea atueleze wakati dc anabaka alikuwa anapiga chabo kutokea dirisha lipi? Au alikuwa anachungulia kwenye tundu la ufunguo?
 
"Rapist" (anayemzini mwanamke bila ridhaa yake/kwa nguvu) nijuavyo ndiye mbakaji. Nauliza kibaka.
 
TUNDU LISSU

Mwanasehria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, alisema mkuu wa wilaya ana mamlaka ya kuamuru mtu aliyefanyakosa mahali ambako hakuna polisi akamatwe.

Kama kuna polisi kwenye eneo la kosa hayo mamlaka hawezi kuwa nayo, na kama akitoa amri hiyo atakuwa anawajibika kutoa maelezo na sababu za kumkamata mtu huyo kwa hakimu wa wilaya.

"Alichokifanya DC wa Kinondoni ni uvunjaji wa sheria na tutamshughulikia hadi ataikimbia hiyo wilaya," alisema Lissu.

KIBATALA

Akizungumzia kuhusu mamlaka ya mkuu wa wilaya kutoa amri ya kukamatwa mbunge, mwanasheria Peter Kibatala alisema amefurahi kutokea kwa kesi hiyo na anaomba suala hilo kwenda mahakamani kama shtaka la jinai.

Alisema kesi hiyo itasaidia kuhoji mamlaka ya mkuu wa wilaya na namna ambavyo anayatekeleza.

"Vyovyote iwavyo lazima tuhakikishe tunawasilisha malalamiko kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ili kupata uamuzi wa nini hasa mipaka kati ya serikali na maafisa wake na wabunge hasa wa upinzani," alisema Kibatala.

FREDERICK KIHWELO

Kwa upande wake mwanasheria wa mbunge huyo, Frederick Kihwelo alisema jambo la msingi katika suala hilo ni kuhakikisha cheo hicho kinaondolewa ili kiweze kuwaacha polisi wafanye kazi zao kwa uhuru.

"Inasikitisha kuona mkuu wa wilaya ni kada wa CCM, mjumbe wa siasa wa wilaya wa CCM na ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hivyo ni bosi wa OCD na ofisa usalama wa wilaya," alisema.

Aliwataka wale waliopewa mamlaka hayo kuhakikisha wanatumia mamlaka hayo kwa busara badala ya kutumia nguvu na jeuri.

Lambalamba sijui kama wanasoma hapo kwenye red?
 
ningekua na uwezo wa kubadili katiba basi wakuu wa mikoa na wilaya wangekua kuanzia miaka 40+
 
Raisi anamsikiliza tu ila kweli anachafua hali ya hewa kwa upinzani kuwaonea bila sababu ya msingi na waandishi wa habari pia kunyanganywa kamera sio kitu kizuri kabisa
 
Si ruksa mtu yeyote mwenye madaraka yeyote yale kumtusi mtu mwingine. Mbunge wa Ubungo kwa kumtukana Makonda Mh. Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kumwambia "kibaka" na mwenyewe alikili kituo cha polisi, anastahili kushitakiwa tungoje sheria ichukuwe mkondo wake. Tusiishi kwa mazoea.
 
neno kibaka sio tusi na kama tusi kwenu nyie mazombi, mahakamani sio tusi, linamaana nzuli tena ya heshima kwa wafungwa.
 
Mpumbavu,mtu amekaa kutatua mgogoro toka asubuhi halafu eti aje kuhatarisha amani?Amani ya nani?Mbona wafanyakazi walikuwa watulivu?mahaba yako na ccm yatakuua kwa kushindwa kuona ukweli!

Ni ajabu kabisa eti Mbunge anaruhusiwa kutukana , tusizidishe mahaba kwa kila jambo.
 
Naona Tundu Lissu na wenzake wana wadanganya...! Matusi ya kubenea yalikuwa yanataka kuhatarisha amani na kuleta vurugu hivyo Paul Makonda alitumia busara ya hali ya juu kumuweka ndani(kumpumzisha) hata Lissu akileta ngebe atapumzishwa..!

Kubenea anapaswa kufunzwa jinsi ya kufanya kazi na serikali na kujua mipaka yake....

Ukilala ukiamka ndio mzee..nyie CCM bwana
 
Last edited by a moderator:
Nyau wewe, mbunge na mkuu wa wilaya, wajua tofauti zao kimamlaka?? Mpumbavu na lofa mkubwa wewe. Huyo Kubenea atakula uongo na matusi yake. Bahati yake Makonda ni mstaarabu na mwenye huruma sana, huyo mbunge alitakiwa ale kipondo cha haja kabla ya kuswekwa upango

Huu ni utumwa wa kichwa POOR TZ yangu
 
Siasa tamu bhana nilifikiri jamaa watakosa kazi ya kufanya kumbe kazi nyingi tu maana ukiwa na wakuu wa wilaya kama huyu jamaa kila siku mok kazini mahakamani hadi raha
 
Naona Tundu Lissu na wenzake wana wadanganya...! Matusi ya kubenea yalikuwa yanataka kuhatarisha amani na kuleta vurugu hivyo Paul Makonda alitumia busara ya hali ya juu kumuweka ndani(kumpumzisha) hata Lissu akileta ngebe atapumzishwa..!

Kubenea anapaswa kufunzwa jinsi ya kufanya kazi na serikali na kujua mipaka yake....

Hivi Dc ndo anajua zaid kuvunjika kwa amani kuliko polisi waliop eneo la tukio?
 
Last edited by a moderator:
Naona Tundu Lissu na wenzake wana wadanganya...! Matusi ya kubenea yalikuwa yanataka kuhatarisha amani na kuleta vurugu hivyo Paul Makonda alitumia busara ya hali ya juu kumuweka ndani(kumpumzisha) hata Lissu akileta ngebe atapumzishwa..!

Kubenea anapaswa kufunzwa jinsi ya kufanya kazi na serikali na kujua mipaka yake....

Mkulu ni amani aliyokuwa Nayo makonda au wale wafanyikazi wa kile kiwanda ndiyo ing?kuwa hatarini? hebu nijuze...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom