Maoni ya Ezekiel Kamwaga kuhusu AG mpya

Maoni ya Ezekiel Kamwaga kuhusu AG mpya

Tee Bag

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
7,220
Reaction score
5,627
UTEUZI WA DR. ADELARDUS KILANGI KUWA AG
Ezekiel Kamwaga
Maoni yangu

Jana usiku Rais John Magufuli amemteua Dk. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali.

Nadhani ni uteuzi unaosisimua. CV ya AG mpya imeshiba na kwa bahati nzuri ni mtu ambaye haogopi kuweka maoni yake hadharani.

Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kwamba nafasi ya AG ni ya kisiasa pia na ndiyo maana bungeni ni mtu muhimu. Nasubiri kuona ladha yake wakati atakapoanza kutekeleza majukumu yake bungeni.

Kwa maoni yangu, Andrew Chenge, ndiye alikuwa AG wa mwisho ambaye kila aliposimama kuzungumza bungeni ilibidi umsikilize.

Frederick Werema hakuwa mbaya lakini alikuwa na jazba. Ndiyo sababu hakusita kumwita mbunge "tumbili". Hutaraji AG kutumia lugha ya namna hii.

George Masaju ni mwanasheria mzuri lakini ule " Uanasiasa" wa AG ulimpa shida kidogo. Hapa, ilikuwa sawa na kutaka kutumia ufunguo wenye umbo la mraba kutaka kufungua kitasa chenye umbo la duara.

Wakti utaamua namna Kilangi atakavyochambuliwa baadaye.

Mazuri


Rais kampa nafasi mtu ambaye wasifu wake hauna shaka. Hapa, amemweka samaki kwenye maji.

Pia, Rais ameonyesha kwamba bado anataka kulifanyia kazi eneo la rasilimali zetu. Hajapoteza focus kwenye hilo.

Kilangi ni mbobezi wa Sheria za Kimataifa na mjuzi wa masuala ya rasilimali. Katika wakati huu ambapo nchi bado inasukumana na wakubwa hawa, Kilangi ndiyo aina ya mtu ambaye anafaa.

Nimezungumza na Godwin Ngwilimi, mmoja wa viongozi wa TLS na Alumni wa Sekondari ya Sengerema kama alivyo Kilangi na amemuelezea AG mpya kama mtu mwenye akili, mzalendo, mbobezi, muungwana na mwenye msimamo. Hizi ni sifa za mtu anayetosha.

Mapungufu

Wakosoaji wa Rais Magufuli wamekuwa wakizungumza kuhusu asivyozingatia mgawanyo wa kijinsia, kidini na kikanda katika utekelezaji wa majukumu yake.

Uteuzi huu, unatoa fursa ya kuibuka tena kwa wakosoaji wake. Labda nieleze kwa mifano kidogo.

Rais ameteua Jaji Mkuu kutoka Kanda ya Ziwa. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ametokea hukohuko, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) wanatokea Kanda ya Ziwa pia ingawa hawa hawakuteuliwa na Rais Magufuli.

Kilangi anatokea Kanda ya Ziwa pia. Nimetaja taasisi hizi kwa sababu zote zinahusika na utoaji wa haki.

Hii inanikumbusha kuhusu rafiki yangu Jamal Malinzi. Siku moja tulizungumza tukiwa Maputo na aliniuliza maoni yangu kuhusu namna watu wanavyomuna huko nje. Nikamwambia watu wanasema unapendelea sana Kagera. Akaniambia atarekebisha hilo.

Siku chache baadaye, aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria wa TFF, Evodius Mtawala, akajiuzulu wadhifa wake huo. Mtu wa Kagera huyu. Nikajua Malinzi kapata fursa ya kurekebisha mambo.

Akamteua Emmanuel Muganyizi (Muga) kushika wadhifa huo. Niliposikia nilicheka tu.

Rais Magufuli alikuwa na fursa ya kumteua mwanamama kwenye wadhifa huo ili kubadili upepo na kuweka historia mpya maana hakuna mwanamama aliyewahi kushika wadhifa huo.

Alikuwa na uwezo wa kumteua pia Mtanzania mwingine mwenye sifa kutoka eneo lingine la Tanzania lakini yeye kaamua vinginevyo.

Wachina wanasema rangi ya paka si muhimu ali mradi anakamata panya.
Labda tatizo letu kama nchi kwa sasa ni kuwa na paka wanaokamata panya wengi na baadaye tatizo likiisha tutaanza kujali kuhusu rangi.

Mpira huu umerushwa kwa AG mpya. Namtakia kila la kheri.

Ezekiel Kamwaga
Dar es Salaam
Februari 2018.
 
Watz kwa kusifiasifia hawajambo

Ova
 
Atakayeamua kupambana na Magufuli kwa kuzungumzia ukanda,hawezi kushinda vita hivyo,na huenda ndipo atachochea hali hii iendelee.Na ikiendelea,wasukuma hawatatatoka madarakani milele..maana wako wengi.Na ccm itaendelea na mchezo huu wa kuteua wasukuma ili iendelee kushinda.
 
Ni vigumu sana kufanya kazi na kufanikiwa chini ya bosi kigeu geu na asiyejua anachokitaka huku yeye akiwa ndie muelekezi na mshauri wa taalum uliyoisomea
Mkuu pokea like, umemaliza kabisa kwa kueleza tatizo liliko. Jamaa anataka ufanye anayotaka, na ukifeli kwa sababu ya maelekezo yake analaumu na kutumbua.
 
Ila jamani kusema huu ni wakati Wao. Dah yani nchi yote wanaimiliki wao
 
Namuweka kiporo huyo mpuuzi Ezekiel Kimwaga anayependekeza ujinga wa watu kupewa nyadhifa na majukumu kwa vigezo vya kijinga vya udini, ukabila, ukanda au umaeneo

Saa hizi ngoja nipumzike
vigezo hivyo ndio linalifanya Taifa liwe moja. ukifata sifa ukipuuzia unajijengea uhalali wa kuchagua wachaga watupu!
 
Ezekiel unatuabisha wana Dar es Salaam! Yaani bado unawaza katika ukanda, ujinsia nakadhalika katika mapambano haya ya kukwepa unyonyaji!? Kwa taarifa yako wakati wa mapambano umuhimu wa nyenzo(silaha) za mapambano ndiyo muhimu bila kujali nyenzo ni ndefu, fupi, nene nyembamba, nzito nyepesi nakadhalika.

Rais wetu mpendwa, Dr. John Magufuli , endelea kufanya kazi kwa nguvu zako zote, sisi watanzania wapenda nchi yetu tunakuunga mkono. Wapuuze wenye kuwaza kama' Eze'
Mkuu these days umekuwaje?
mbona zamani ulikuwa unaongea vitu vya maana sana!
 
Kusifia upate kuteuliwa, more posts are needed to make a target! Jitahidi, kila kheri!
 
Mkuu pokea like, umemaliza kabisa kwa kueleza tatizo liliko. Jamaa anataka ufanye anayotaka, na ukifeli kwa sababu ya maelekezo yake analaumu na kutumbua.
Raisi ndiye amepewa dhamana na wananchi katika kuwaongoza na kuwafikisha kwenye mafanikio. Naye kwa dhamana aliyonayo, pamoja na ilani ya chama chake, ana maono yake na ambayo wateule wake wanapaswa kuyafanyia kazi ili mwisho wa siku taifa lifikie kwenye matamanio yake!
Unapokuwa umeteuliwa, unachopaswa kufanya ni ku - tune taaluma yako kwenye utekelezaji wa maelekezo ya kiongozi mkuu pamoja na ilani ya chama tawala ili kilichoahidiwa kwa wananchi katika kuboresha hali zao za maisha, kifikiwe! Kinyume chake, hata kama wewe ni mubobezi wa taaluma gani, hufai kuwepo kwenye hiyo nafasi!
Kwa mktadha huo hapo juu, naamini raisi yuko sahihi katika panga pangua yake ili kumpata mtu sahihi mwenye kuendana na maono ya taifa!
Tujitafakari!
 
Hakika kila lifanywalo na mwanadamu lina mwisho wake

Hata kama CV itajaza magunia na akawa MTU wa KUFUATA MAAGIZO BASI HAKUNA KITU NI BORA HATA KUMPA HATA KIBAJAJI AU BASHITE WATAFUATA TU MAAGIZO TOKA JUU

Naendapo atafuata elimu yke na UHAKIKA MWAKA MMOJA UNAMTOSHA TU ATAKUWA AMETUMBULIWA. UKIFUATA UTARATIBU KTK UTAWALA HUU WW NI MCHOCHEZI

Watanzania wengi wanashangilia tu wakati sheria zinavunjwa na haki za wengi zinapotezwa. Aje atuambie nchi hii inatawaliwa kijeshi? Kwann hata mikutano tu hakuna. Serikali ikikosolewa tu iwe gazeti TV ama redio Unafungiwa kwa MTU unaangalia Nissan jeupe.
Aje atueleze FAO LA kujitoa
 
Back
Top Bottom