Maoni ya Ananilea Nkya kuhusu hotuba ya Dr. Slaa

Mama ukaskazini unanfanya asiwe na fahamu tena za kutambua mambo. Jamani hatari hii. Mungu saidia Tanzania hawa watu wasipate nafasi.....

..akili za kushikiwa shida sn,mlidhani wote wananunulika km mlivyomnunua huyo dokta mihogo?!
 
Na Ananilea Nkya

Nimeisikiliza hotuba Dr Slaa kwenye youtube--nimeungana na wananchi ambao wamesema Dr Slaa kwa kujua au kwa kutokujua amekubali kutumika kuyumbisha maelfu ya wananchi wanaotaka mabadiliko nchini na kwa hiyo amejichafua mbele ya Watanzania.

Dr Slaa anapaswa kujua kwamba mabadiliko ni lazima kwa sasa na hayazuiliki tena maana nchi ilipofikia sasa Septemba 2015, wenye ari kubwa ya kuleta mabadiliko ni wananchi wenyewe kupitia sanduku la kura hapo tarehe 25 Oktoba.

Pengine Dr Slaa hakujua kuwa wananchi wanaotaka mabadiliko ya uongozi nchini walikuwa wameshamsahau maana tangu alipoacha kuonekana hadharani hasa wakati wa kumtambulisha Edward Lowassa kama mgombea Urais wa UKAWA--muungano wa vyama vinavyopigania kuingia madarakani vikiwa na ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi, wengi walishajua kuwa Dr Slaa hayupo tena upande wa wananchi.

Alichokisema Dr Slaa kwenye hotuba yake ya kile alichokiita 'kuachana na siasa za vyama' ni kajichafua yeye mwenyewe na kuharibu heshima aliyojijengea kwenye jamii.

Kwa mfano Dr Slaa alisema eti aliweka msingi kwamba angemkubali Edward Lowassa kugombea Urais iwapo angeondoka CCM na mtaji wa wabunge 50 kuhamia UKAWA ili wagombee ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD- vyama vinavyounda UKAWA.

Hivi Dr Slaa aliona vijana wanaochakarika kwenye vyama vinavyounda UKAWA wao hawataki kuwa wabunge? Hawastahili nao kufaidi mshahara wa shilingi milioni 10 kila mwezi na kiinua mgongo cha zaidi ya shilingi milioni 200 baada ya miaka mitano ?

Hebu fikiria wabunge wa CCM ambao wengi wamekuwa bungeni miaka kumi, ishirini wengine miaka thelathini na zaidi. Ni matajiri kiasi gani leo hii? Hivi watu wa aina hiyo kweli wanaweza kuondoka kwenye chama chao kwa wingi kiasi hicho na kuamua sasa kupigania kuondoa mfumo unaowatajirisha wao ili wananchi wengi masikini nao watajirike?

Watakuwa na shida gani wakati kwenye chama chao hata kama mtu umekosa kuteuliwa kugombea ubunge malofa wakishaichagua CCM serikali ya CCM inawagawia kazi za ulaji watu waliokosa ubunge? Kwani wewe hujamsikia Mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli akiwatangazia wale walioanguka kwenye kura za maoni ubunge CCM kwamba wasijali anazo kazi tele za kuwapa akichaguliwa Rais?

Kwa mtazamo wangu--walioamua kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA kama kweli dhamira yao ni kushirikina na UKAWA kupigania kuingiza serikali ya UKAWA madarakani ili kuandika Katiba Mpya ya wananchi--watu hao wanastahili pongezi maana watakuwa wamefanya maamuzi magumu na muhimu ya kuwezesha wananchi wengi kuondoka kwenye umaskini unaosababishwa na serikali ya CCM.

Hivi Dr Slaa kweli anadhani mabadiliko ya kuchagua serikali itakayoandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi yatatokea nchini kwa wabunge wengi wa CCM kuondoka CCM –kujiunga UKAWA--wabunge ambao waliizika Rasimu ya Katiba ya wananchi pale Dodoma 2014 huku wakiwa wanalipwa kila mmoja shilingi laki tatu kila siku kwa takriban miezi mitatu?

Hivi Dr Slaa hajui kwamba wanaotaka mabadiliko ni mamilioni ya Watanzania wakiwepo wanachama wa CCM wanaoumizwa na umaskini ambao chimbuko lake ni mifumo iliyowekwa na serikali ya CCM--mifumo inayotajirisha watawala wachache huku mamilioni ya wananchi wakiwa mafukara?

Kwa mtazamo wangu, wananchi wengi wakitafakari hatua aliyochukua Dr Slaa na maneno aliyoyazungumza hadharani watabaini kuwa Dr Slaa amejidhihirisha kuwa ni mtu mbinafsi.

Zaidi watabaini kuwa Dr Slaa pengine aliingia kwenye upinzani akidhani siasa ni kama kazi nyingine. Kumbe siasa hasa kuwa kwenye chama cha upinzania ni kujitoa hata kama kuna kuumia kiasi gani –hadi lengo la ukombozi wa pili wa taifa hili--ukombozi wa kuondoa mifumo inayowafukarisha wananchi ing’olewe.

Kwa maoni yangu, kama Dr Slaa angekuwa ameingia kwenye siasa kupigania ukombozi wa wananchi--kamwe asingekubali kukaa pembeni sasa--tena baada ya yeye mwenyewe kukubali Lowassa aingie UKAWA mradi awe ni mtaji na si hasara. Kibaya zaidi asingekuwa upande wa watawala wanaofukarisha wananchi eti kwa sababu Lowassa alishindwa kuleta UKAWA mtaji wa watu wa kugombea ubunge.

Pengine Dr Slaa amekuwa na tafsiri finyu kuhusu mtaji wa siasa. Siamini kuwa vyama vinavyounda UKAWA vina uhaba wa watu wenye uwezo wa kuwa wabunge. Hivyo mtaji muhimu ambao Dr Slaa angeutaka kwa Lowassa ni wapiga kura. Angejiuliza je huyu Lowassa anakubalika kwa wapiga kura?

Jibu kama Lowassa anakubalika kwa wapiga kura au la Watanzania wenyewe wanalo jibu na hadanganyiki mtu hapo. Watanzania wameshuhudia mafuriko ya Watanzania wanaomuunga mkono LOwassa. Hayo mafuriko ya wananchi ni mtaji wa wapiga kura ambao Lowassa ameongeza UKAWA na hicho ndicho kinachowasumbua watawala.

Tena Watanzania wanaomuunga mkono Lowassa hawajakosea maana hata Mwalimu Nyerere alitamka hadharani mwaka 1995 kwamba Lowassa ni mtu mwenye dhamira na uwezo wa kuiongoza Tanzania.

Isitoshe wananchi wanamuona Lowassa kuwa ni mtaji muhimu maana kwa kuhama CCM amehamasisha nguvu kubwa ya umma katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi.

Dr Slaa alisema eti kwenye familia yake wanakula mhogo na maharage. Hivi familia inayokula mhogo na maharage (yaani kwa sababu ya umaskini wa kikwelikweli) inaweza kumruhusu baba ambaye alijibainisha kuwa ni kamanda wa mapambano ya wanyonge awageuke mamilioni ya Watanzania ambao hata mhogo na maharage hawapati na hivyo siku nyingine hulazimika kulala njaa?

Kama Lowassa angeingia CHADEMA na asigombee Urais badala yake CHADEMA na UKAWA wangemteua Dr Slaa kugombea Urais, je Dr Slaa angetamka maneno aliyoyatamka? Hata kama Dr Slaa angekuwa na uadilifu kama malaika angetoa kauli zinazofanana na zile wanazotoa watalawa wa CCM dhidi ya mamilioni ya Watanzania wanaotaabika kwa umaskini?

Hivi Dr Slaa ameamua kuungana na serikali ya CCM kudanganya wananchi kwamba tatizo la umaskini unaosumbua mamilioni ya Watanzania chanzo chake siyo serikali ya CCM bali ni Lowassa na hivyo Lowassa akiingia madarakani ufisadi utaongezeka nchini?

Kimsingi Watanzania wa leo HATUDANGANYIKI. Zaidi sana Mungu wa wanyonge ni mnyofu sana hatawaacha Watanzania mwaka huu—mwaka wa mabadiliko.

Ninawatia moyo Watanzania wote mkiwepo wana CCM mnaoumizwa na hali ya umaskini miongoni mwa wananchi wengi nchini kwetu msikate tamaa wala kuogopa kama akitokea kiongozi mwingine wa UKAWA akageuka wananchi kama Dr Slaa na Prof Lipumba kabla ya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015 ninyi songeni mbele, mabadiliko yanawezekana.

Kimsingi ni kila mtu kutambua kuwa kuna njama nyingi zinazofanyika kwa lengo la kuvuruga wananchi ili waogope au wapuuze kufanya mabadiliko.

Sote tuwe macho, hakuna kuchoka, hakuna kuogopa .Mabadiliko ni lazima hayazuiliki. Mungu ibariki Tanzania.

Narudia kusema mimi sina chama chochote cha siasa ninachofungamana nacho. Ninachopigania ni maslahi ya mamilioni ya Watanzania masikini (malofa) kwa utawala mbovu wa serikali ya CCM.

Ninaruhusu mwenye kutaka kuchapisha makala hii afanye hivyo maana historia itatuhukumu mmoja mmoja na kama kundi linalopigania mabadiliko Tanzania.

Kwa maswali niandikie: ananilea_nkya@...


Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@...

Mwandishi anakiri kwamba, Dr. Slaa amesahaulika tangu kutambulishwa Lowassa kuwa mgombea wa UKAWA. Kama hilo ni kweli, kwa nini aandike andiko refu namna hii kwa mtu asiyekua na madhara yoyote?

Kwa nini asielekeze mashambulizi kwa Magufuli? Very contradictory.
 
Mimi naamini mtu yeyote mwenye fikra za kutulia, huwa kuna wakati anakaa chini na kutafakari. Kwa nini Dr. Slaa ajifikirie kuwa kila wakati ni yeye tu ndio yuko sawa?

Hebu ajiulize ni institutions ngapi ameshahitilafiana nazo, huko kote wabaya ni wengine tu?

1. Kanisa Katoliki, the biggest institution number-wise
2. Ndoa, taasisi ya watu wawili
3. CCM, taasisi yenye watu wa aina yake
4. CDM, taasisi ya maendeleo

There is a day that he will walk away from his own body
 
Nkya katika maisha yako yote hukua unasimamia uadilifu bali uchaga hilialielewak sana KAMA ni madiliko hata wewe tunataka mabdiliko
 
Kama kujitambua ni kukubali kila kitu kinachosemwa na mtu wa kaskazini bila kuhoji mantiki ya kauli yoyote aheri nisijitambue. Kama kukataa ukabila wa wakabila wa kaskazini ni ukabila basi aheri niwe mkabila. Kama macho yangu yananiambia rangi hii ni nyekundu wewe unaniambia niseme ni ya kijani sitasema ni ya kijani nitasema ni nyekundu. Kwa kifupi nitasimamia ninachokiamini mimi siyo unachokiamini wewe. Napenda mabadiliko, lakini pia napenda kujua, aina ya mabadiliko, anayeyaleta na namna yanavyokuja. Mabadiliko ya kipurure, yasiyoangalia yanakuja na nini (uzuri au ubaya) hayawezi kukubalika na any serious great thinker. Mabadiliko yanayoletwa na kusimamiwa na mtu asiyejua hata tafisri ya 'Change management' Kama sitaki ufisadi, fisadi hawezi kusimamia mabadiliko ninayoyataka. Ninaposema sitaki ufisadi maana yake simtaki mtu yeyote fisadi, siwezi kumkataa huku nikimkumbatia. Nitaonekana nimechanganyikiwa.

This is non sense, give us a break! unataka Mabadiliko yenye mwelekeo unaoleweka wa CCM na Mafisadi wote huku unakataa Mabadiliko yanayoongozwa na Fisadi mmoja!
 
Asante sana mama. Nani kama mama? Waambie wanaotelekeza watoto na wake zao. Eti wanajiita waadilifu. Laana ya usaliti itaendelea kumwandama babu slaa. Kasaliti upadre, kasaliti mke, kasaliti ccm, kasaliti CDM na kasaliti Watanzania wanaotaka mabadiliko. Sisi tunasonga mbele na mabadiliko ni lazima. Mabadiliko Lowassa! Lowassa mabadiliko! Hatudanganyiki. Miaka 54 ya mateso inatosha. Vote for Ukawa, vote for Lowassa.
 
Mwandishi anakiri kwamba, Dr. Slaa amesahaulika tangu kutambulishwa Lowassa kuwa mgombea wa UKAWA. Kama hilo ni kweli, kwa nini aandike andiko refu namna hii kwa mtu asiyekua na madhara yoyote?

Kwa nini asielekeze mashambulizi kwa Magufuli? Very contradictory.

Huyu mama ningemuona wa maana na mwenye busara kama angezungumzia ile kauli ya Lowassa kuhusu Kina Babu Seya na ubakaji.
 
One approved fisandi against many assumed fisadi and the approved fisadi was the leader of the assumed fisadis. Where do you go about my dear boy? He was rejected cause he was ruining the party and he is going to ruin the other party where he is, which actually was doing better before his entrancement. Stay tuned my dear boy you will tell me aftermath.
This is non sense, give us a break! unataka Mabadiliko yenye mwelekeo unaoleweka wa CCM na Mafisadi wote huku unakataa Mabadiliko yanayoongozwa na Fisadi mmoja!
 
Kulinda midomo yetu ni TUNU kubwa sana ambayo hujenga heshima binafc na taasic zetu. Mh Lowasa amejaaliwa hili kwa miaka 8 amekaa kimya juu ya tuhuma zinazomkabili. C kweli kuwa hana maneno ya kutosha kuwachafua wapinzan wake. Dr. Slaa amechemka sana kwa kudhan kuwa atatumia mavi ya kale kumchafua Lowasa. Busara ya kawaida imemshinda na alichokikusudia hakijatokea na hakitakuja kutokea, waliomtuma watafute mbinu nyingine kabla muda haujawaacha. wajue kuwa muda hauwasubiri. Watz wameamua kugeuka inaweza kuhitaji miezi zaidi ya 20 ambayo haipo. Polen sana sisiem
 
Ni mtizamo wake tu kama mtz

Humu jf nimegundua Id ambazo ni kongwe nyingi hazimtetei ila kuna baadhi zinamtetea kwa maslahi yao zilizojaa mpya tu

Vijana nendeni field sio kwenye mitandao hapa ni kakikundi kadogo sana ka watu

Hii ndo siasa za tz na watz ni unafiki na wanafiki tu mwanzo mwisho
 
Pole sana mama ccm waachie wenyewe, slaa anatumia uhuru wake, wewe shabikia Ukawa usumbuliwi, kila mtu navane mama pole sana umetumia nguvu nyingine siasa ni giriba mama
 
Ni mabadiliko gani anazungumzia mwanaharakati huyu? Kwani Lowasa anataka mabadiliko? Mpenda mabadiliko hawezi kupigania Urais kupitia CCM. Lowasa anapitia CHADEMA kwa vile tu ameshindwa kupitia CCM. Chaguo lake la kwanza ni CCM.

Lowasa katoka CCM na kikundi cha wana CCM waliokuwa wafuasi wake. Hicho kikundi ndicho kinataka kitawale sasa kwa kupitia CHADEMA.

CCM imemeguka vipande vipande. Kipande kimoja kinataka kuchukua Urais kwa tiketi ya Ukawa na kingine kinataka kuchukua Urais kwa tiketi ya CCM.

Hatutapata mabadiliko kama tutawachagua Lowasa au Magufuli.
 
One approved fisandi against many assumed fisadi and the approved fisadi was the leader of the assumed fisadis. Where do you go about my dear boy? He was rejected cause he was ruining the party and he is going to ruin the other party where he is, which actually was doing better before his entrancement. Stay tuned my dear boy you will tell me aftermath.

He can't spoiled UKAWA! and he is not worse than the whole system that is spoiled.
 
Back
Top Bottom