GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,030
- 126,474
Wakati watu wakihangaika na kupoteza muda huku wakiumiza vichwa kwa kutaka kujua nani ni rais ajaye wa tanzania 2015 - 2020 na pengine 2020 - 2025.
Kwa habari nilizozipata jana usiku kutoka jikoni kabisa ni kwamba Rais wa Tanzania atatoka katika watu hawa watajwa hapa juu na leo naweka nadhiri kuwa kama hatotoka kati ya watu hawa watatu nitakaowataja hapa chini naomba au nitaomba watanzania wote mnipige mawe mimi gentamycine hadi nitokomee kabisa duniani.
Majina hayo ni haya yafuatayo na majina haya yatabakia baada tu ya kufanywa screening katika vikao vya chama.
1. Samuel sitta - Huyu Atachaguliwa baada ya Bernard Membe kuenguliwa ili kuvunja makundi ndani ya chama hivyo
Membe na wafuasi wake wote watamuunga mkono mzee Samuel Sitta kwa makubaliano ya kwamba Sitta akiwa rais basi Membe atakuwa running mate wake na baadae Makamu wa Rais.
2. Dk. John Nchimbi....Huyu Na yeye atachaguliwa na kikao cha chama kubakia ktk hao watu watatu wa mwisho. Kitakachotokea hadi John Nchimbi kupitishwa kugombea urais, ni baada ya mwenye nia hiyo Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa kuenguliwa ili kukiokoa chama na kuvunja makundi ndani ya chama ambapo mzee lowassa atahakikisha kuwa mtu wake anayemwamini, John Nchimbi atapita na kuwa Rais kisha kumteua yeye kuwa running mate wake na baadae makamu wake wa rais na mpango huu sasa unaendelea kichinichini na kuna uwezekano mkubwa Rais wa Tanzania akawa ni Dk. John Nchimbi kutokana na kwamba Lowassa atakuwa na ushawishi mkubwa katika jamii kwa wakati huo.
3. Abdurahman Kinana - Huyu na yeye atapitishwa kuwa mmoja wa wale watakaobakishwa katika wale watatu bora wa mwisho. Na kwa msiojua ni kwamba hizi ziara anazozifanya mzee Kinana japo anasema kuwa ni za kukiimarisha chama lakini ukweli ni kwamba hizi ziara mzee Kinana anazitumia kujiimarisha yeye ili wakati wa kampeni endapo atabakia yeye basi kazi kupiga kampeni kwake itakuwa ni nyepesi kutokana na kwamba tayari wananchi watakuwa wameshamjua vya kutosha.
Na ili kuzoa kura nyingi za akina mama au wanawake ambao ndiyo wengi hapa nchini, Mzee Kinana atamteua mama Asharose Migiro kuwa running mate wake kisha baadae kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Uhakika wao Ki-asilimia;
Dk. John Nchimbi..................40%
Abdulrahman Kinana..............35%
Samuel Sitta.......................25%
Hivyo Rais wa Tanzania atakuwa ni Dk. John Nchimbi mtake msitake, na mkakati huo unasukwa kitaalamu sana.