Maoni na Ushauri ili kuboresha shughuli za huduma ya Udalali

Maoni na Ushauri ili kuboresha shughuli za huduma ya Udalali

FAJES

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
723
Reaction score
658
Wakuu heri ya kuiona siku hii ya leo. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu aliye Mkuu zaidi ya uwezo wetu wa kuona, kusikia, kuhisi, kunusa na kuonja.!

Kama tujuavyo kuwa, Udalali ni shughuli kama zilivyo shughuli nyingine, ikiwa na lengo la kuwaunganisha muuzaji na mnunuzi wa huduma.

Vilevile ni ukweli usiopingika kuwa, huduma ya udalali imekuwa msaada kwa watu mbalimbali haswa linapokuja suala la upatikanaji wa huduna/bidhaa kwa haraka na urahisi zaidi.

Pamoja na tasnia hii kustawi na kuwa msaada, lakini zipo changamoto mbalimbali inazokabiliwa nazo. Changamoto hizi si kwa upande wa mtoa huduma pekee bali hata kwa mpokea huduma. Zipo changamoto za gharama kuwa kubwa, uaminifu, customer care, n.k.

Kwakuwa tasnia hii ni muhimu kwa jamii, tukunane hapa Wadau (Watoa huduma na wapokea huduma) ili tujadiliane kwa pamoja namna ya kuboresha huduma hii muhimu.

Hivyo karibuni sana Wadau kwa maoni na ushauri.
 
Punguzen commission yenu kwenye mali mnayomuonyesha mteja hii itasaidia sana kuowaongezea wateja
 
Punguzen commission yenu kwenye mali mnayomuonyesha mteja hii itasaidia sana kuowaongezea wateja
Well, unadhani commission kiasi gani itakuwa fair na reasonable.? Tumezoea huduma nyingi hutolewa kwa makubaliano ya malipo ya fedha ya mwezi mmoja kwa gharama ya kupanga. Unaposhauri jaribu pia kuwa fair maana kupata nyumba si kazi rahisi pia, inaweza kuwa imepitia kwenye mikono ya watu wengi na kila mtu anategemea commission hiyohiyo. Mara nyingi ni kuwa fedha anayotoa mteja siyo pesa ya mtu mmoja, nyuma yake kunaweza kuwa na watu zaidi hata ya watano.
 
Karibuni kwa maoni na ushauri..
 
Back
Top Bottom