Makisha
Member
- Oct 19, 2016
- 24
- 52
Wakuu habari za wakati huu.
Naomba niwasilishe maoni yangu juu ya tukio hili la kuhuzunisha lililotukuta, nina huzuni kubwa toka nimesikia tukio hili nafsi yangu haina furaha kabisa.
Kama mzazi nimejivika uhusika wa kifo cha watoto wale ikiwa kama mmojawapo ni wangu kweli maumivu yake hayafikiriki kabisa .
Kirahisi tu watu wanasema R.I.P. hakuna kauli naichukia kama hii hususani kwenye matukio kama haya. Watoto wasio na hatia wamekufa kama wadudu sisi tunakimbilia rip, hata bila kuhoji!!!!!
Hapo lazima kuna uzembe tu umefanyika KAMA SIO kwa boss(mmiliki), Fundi anae fanyia service gari au DEREVA. Na ukizingatia magari yanayo beba watoto wetu kuwapeleka shule yalivyo hayana service ya maana kabisa mengi mabovu. Japo hata tufanye nini hawatarudi kua hai but tujifunze kupitia hili.
Tuanzie hapa tatizo lilikua wapi hadi likatokea hili. Kama palikua na uzembe mahali tuushughulikie, Then tuhakikishe tunaweka mikakati thabiti ya kuwalinda watoto wetu, tuwawekee mazingira salama ya elimu. Tuliwaachia uhuru sana wamiliki wa mashule na walimu kuamua na kucontrol maisha ya watoto wetu.
Hususani kwenye swala la usafiri ambalo leo ndio limetuletea kilio cha historia. Watoto wetu wengi wanapandishwa magari mabovu na hawakai kiutaratibu mzuri waendapo au watokapo masomoni, utakuta gari bovu then limebeba watoto wengi kupiliza idadi halisi, utakuta gari ya watoto 12 imebeba hata watoto 24. Watu hutufutilii hata tukifuatila hatuongei tunaona ni kawaida Leo yanatokea haya tunakimbilia REST IN PEACE Kweli!!!!!Mfn; tu hapo kwenye hilo tukio utakuta kuna mzazi hata hajui mtoto wake alipanda usafiri wa namna gani, wakati anaenda ziara ya mbali.
Plz naomba kila mtu atimize wajibu wake, USALAMA WA MTOTO UNAANZIA MIKONONI MWAKO MZAZI ndio wangine wafuate kwa utekelezaji.
Tunaomba Mungu awarehemu marehemu wote na awatie nguvu wafiwa. Na wengine tujifunze kupitia hili tuombe lisitokeee tena. (Nawasilisha japo kwa kubwabwaja kwa jazba)