comrade_kipepe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2019
- 3,303
- 4,237
Nipo nacheki hapa msiba wa Ndugulile, kuacha watoto wawili tu, pamoja alikuwa ana uwezo wa kipesa na cheo lakini kaishia kwenye watoto wawili, watoto wawili hawa naona kawakuza na kuwasomesha kwenye shule za gharama inawezekana nje ya nchi maana hata Kiswahili chao ni broken sana wanakuwa kama sio watanzania.
Lawrence Mafuru nae nadhani aliacha watoto wawili tu.
Swali kwa makapuku wenzangu, hivi Sisi maskini tunazaa watoto wengi ili iweje? Na utakuta pengne hata uwezo wa kuwahudumia tuu kikamilifu kwenye elimu na gharama za kila siku hatuwezi, nini maana ya hii?
Nahis NI vizuri kuzaa watoto kulingana na kipato chako, ambao utawamudu vizuri, utakaowapa elimu ya uhakika sio hii ya kuunga unga.
Sisi maskini tunawaza eti tukizaa watoto wengi ndio hao badae watatusaidia, wewe mzazi somesha mtoto, hudumia kwa kadiri ya uwezo wako maana ni jukumu lako, badae akipata maisha mazuri NI yeye sasa atajua atakusaidiaje, ndio ile utakuta wazazi wananunia wakwe zao wanaona kama wao ndio wanafanya wasipewe pesa na mtoto wao.
Tuzae Kwa mahesabu, utakuta mtu ana watoto wanne, halafu kapanga chumba na sebule, sasa jiulize hapo ndani wanaishije, tuwekeze nguvu kwenye kujenga uchumi Kwanza na kuzaa kwa akili.