Maoni: Chukua hatua kuhusu Corona

Dim Ray

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
318
250
Habari zenu wana jamvi. Nachukua nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kunipatia uhai. Kwa wale wagonjwa tumuombe Mungu.Matumaini yangu mapambano dhidi ya Corona yanaendelea...

Leo nimeona na mimi nitoe maoni yangu kuhusu gonjwa hili la Corona. Tukiachana na conspiracies zinazoibuliwa na watu kuhusu Corona, kama uwepo wa 5G umepelekea kuwepo kwa Corona mara sijui imetengenezwa China mara U.S.

Tuachane na hayo yote, tufanyeje hatuwezi tukalialia kupambana kujua ugonjwa umetokea kwa sababu ya nani. Ukweli ni kwamba janga hili limetukumba ,sehemu mbalimbali za dunia zinaathirika, cha msingi ni kupanga strategy kuzuia na kupambana na idadi ya vifo na maambukizo. Tukiachana na propaganda ni kwamba dunia inapumulia mdomo kama keba(mbwa) alokimbia kwa mda mrefu. Penda usipende ukweli ni kwamba hakutakuwa na mda ambao utaambiwa kwamba hali ni mbovu na mtu yoyote ,pambana kwa upande wako.

Zifuatazo ni strategies za kuzitumia kupambana na corona.

1.Acha mapuuzo.

Wa Tanzania wengi (si wote) wanapenda kujipa moyo na kupuuzia hata mambo ya msingi. Ugonjwa upo jamani acheni story uchwara za vijiweni kwamba haidhuru waafrika utapukutika vibaya mno.

2. Jiandae kwa majanga ya dharura.

Hali inavyoendelea ni kwamba uwezekano wa kutokea matatizo yanayohitaji pesa hapo mbele ni jambo la kawaida. Cha msingi jitahidi at least kuwa na structured plan ya kujisaidia mda wa matatizo, umewai waza gonjwa hili likitupiga mpaka 2021 hali itakuwaje " maybe it is home(Earth) to stay".

3.Epuka nasema Epuka narudia Epuka mikusanyiko.

Mambo ya kuwa loose kuhusu kuepuka mikusanyiko haitakusaidia, unajikaanga mwenyewe huwezi jua yawezekana huyo huyo unayemuamini ni muathirika wa Corona. Cha msingi acha kabisa kuweka mikusanyiko ya ovyo ovyo maisha hayana alternative.

4. Usimjaribu Mungu

Hapa ninaongea na wale washika dini Moslems and Christians jamani tusi "test" mitambo ya corona, Mungu anasaidia lakini fuata taratibu za afya. Inakera kuona waumini wa dini tajwa hapo juu kulilia imani yao kuwa itawa "save" wanasalimiana kawaida kwa mikono yao na kufanya mikusanyiko na kudai Mungu muweza wa yote anawasaidia.

Men be serious unajikata kidole makusudi ukifikiri nitakupaka hata dawa na kukufunga bandeji kwa kweli?, nimeongea haya baada ya kumshuudia mchungaji wa kanisa letu siku ya jumapili akisaliminiana na almost watu zaidi ya kumi kwa kushikana mkono ingawa alivaa barakoa, sidhani kama Mungu yupo tayari kusaidia watu hopeless kama hawa.

I' m possible
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom