Maombi ya msaada wa kumaliza Ada

Kwanza pole lakini njia unayoitumia huenda ikakukwamisha,
1)Moja maelezo yako hayaelezi unahitaji kiasi gani
2)Ingekua rahisi zaidi harakati hizi ungeanzia ndani ya familia/ndugu/ukoo lakini kama umeshafanya hivyo na ikashindikana ni sawa.
3)Nyumba za ibada ni njia rahisi zaidi kufanikisha tatizo lako
4)Wenzako wanapotoa maombi ya namna hio hua wanaeleza na kutoa uthibitisho wa kulipa deni na wanasema watalipa lini huku wakiacha vyeti vyao mfano cha cheti cha form four/six kama dhamana.
5)Hua wanajaribu kuthibitisha hitaji lao kwa kua vielelezo vya vyuoni wanaposoma mfano statement of result kama ya mwaka wa kwanza na wa pili,nakala ya vitambulisho vyao vya chuo,kwani siku hizi watu hawaaminiki wengi wamekua waongo maisha yamekua magumu hasa utawala huu wa awamu ya tano.
Huu ni ushauri tu,kila la heri!
 
pole sana ndugu yangu kwa tatizo hilo ila mungu yu pamoja nawe kwakua ulianza na umefikia hatua hiyo naamini utafanikiwa na kumaliza masomo yako,ushauri wangu ni1.jaribu kushirikisha ndugu zako wakaribu kama wapo iliujue waowatakusaidia nn? 2.wakishindwa ndugu jaribu kumshirikisha rafiki yako wakaribu ambaye unamuamini kwa%mia 3.yakishindikana yote hayo jaribu kwenda kwenye nyumba za ibada kama kanisani au msikitini lakini angalizo kuamuaminifu sana kwahilo unalohitajia mwisho au kama uliamua kutumia pesa ya ada ambayo ulipewa na wazazi jaribu kufaiti ili ipatikane hiyopesa ya watu ya ada au ikiwezekana azima kwa washkaji naamini kiwangokilichibakia unadaiwa nikidogo sana so fanya hivyo kk niushauri tu ndugu mungu atakusaidia kk pamoja sana.
 
Mdg wangu ushauri uliopewa ndiyo sahihi, kukwama ni jambo la kawaida hususani kwa wanaojua mapito, hata matajiri unaowaona leo nao yamewasibu mengi.
Kama yalivyo tolewa maoni hapo juu, jipambanue kwa kujiweka wazi kuwa, kwa aliye tayari kwa msaada hitaji lako ni ada kulipwa, toa namba ya Account ya chuo au ushahidi wa chuo unachosoma.
 
Back
Top Bottom