Maombi ya kujiunga vyuo vikuu Tanzania sasa kwa 'message' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maombi ya kujiunga vyuo vikuu Tanzania sasa kwa 'message'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwenda_Pole, Jan 20, 2010.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imeanzisha mfumo mpya wa wanafunzi kuomba kujiunga na vyuo vikuu ambapo hivi sasa wanafunzi wanatakiwa kuomba kwa kutuma ujumbe kwenda namba 15789 au kutumia mtandao na maombi yote yatapokelewa na TCU.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Mayunga Nkunya, alisema kwa kupitia mfumo huo, waombaji hawatatakiwa kutoa vyeti vya majibu yao wakati wa maombi kwa kuwa TCU itakuwa inayapata moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani nchini( Necta).

  Lakini alisema kwa wale wanafunzi watakaoomba kutoka shule za kimataifa watatakiwa kupeleka majibu yao Necta ili yakahakikiwe kabla hawajatuma maombi yao.

  ``Wanaotakiwa kuomba ni wale waliomaliza kidato cha sita, ndiyo watakaoweza kutumia mfumo huo, na ni kwa kuanzia wale waliomaliza mwaka 1988 hadi leo,``alisema Prof Nkunya na kuongeza;

  ``Wale ambao hawakumaliza kidato cha tano au wamepitia elimu ya watu wazima hawataweza kutumia mfumo huo kwa kuwa haiwaruhusu, ``.

  Kuhusu majibu alisema nayo yatatolewa kwa ujumbe mfupi au mtandao na kwamba ni muhimu waombaji wakaambatanisha namba mbili za simu ambazo zinapatikana au email kwaajili ya kurahisisha mambo.

  "Ili wanaotaka kutuma maombi waweze kuelewa mfumo huu, TCU imeandaa kitabu chenye maelezo kamili kuhusu namna wanafunzi wanavyoweza kufanya na vitasambazwa katika mikoa yote, kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu, wizarani, Nacte, ofisi za bodi ya mikopo zilizipo mikoani na Dar es Salaam na ofisi za TCU,"alisema.

  Profesa Nkunya alisema pia katika tovuti ya TCU, wizara ya elimu, Nacte, vyuo vya elimu ya juu na bodi ya mikopo maelekezo hayo vinapatikana.

  Alisema wanafunzi watakaotuma maombi watatakiwa kuomba programu 12 tu kwa taasisi tofauti kama mfumo huo ulivyoandaliwa, lakini katika kufanya hivyo muombaji anatakiwa kuchagua programu nane kwenye taasisi tofauti na programu tatu kwa taasisi moja.

  Prof Nkunya alisema mfumo huo unaanza kutumika kuanzia mwaka wa masomo wa 2010/2011 na wanaotuma maombi wanatakiwa kuanza kufanya hivyo kuanzia Februari 15 hadi Mei 31 mwaka huu.

  ``Hakuna maombi yatakayokubaliwa baada ya mwezi Mei 31 mwaka huu,``alisema Profesa Nkunya.

  Alisema waliotuma maombi watapewa majibu yao June 4, na watatakiwa kuhakikisha majibu hayo hadi ifikapo Juni 11 mwaka huu.

  Alisema mfumo huo umeigharimu TCU kiasi cha Sh 1 bilioni ambazo zimetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

  Source: Wanazuoni forums
  ................................................

  Weka Maoni yako, unafikiri nii ndio njia ya rahisi zaidi ambayo hawa jamaa watumie?
  angalia ishu ya gharama, pamoja na uhaliasia wa mfumo huu katika utekelezaji
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hii kitu inawezekana ni maridadi kwa upande wa kupunguza kufojiwa kwa vyeti, sina uhakika na hili anyway!
   
 3. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hawa TCU kwanza Tovuti yao haipatikani na sina uhakika kama wana wafanyakazi makini katika kitengo chao cha TEKNOHAMA(ICT)!!!hili nalo linaweza kuleta Mizozo kama ya bodi ya Mkopo.
  Maana wamekuwa na mipango mingi na yote utekelazaji wake ni mdogo!!!Nakumbuka mwaka 2008 ilitokea Idadi kubwa sana ya wanafunzi ambao walichaguliwa vyuo zaidi ya kimoja!!!wakasema sasa inabidi maombi yote yapitie TCU ila hilo halijafanyika hadi hv leo!!!!!!!!!!!hivi huo muundo ni wa kuleta Tija au ni wa kuzidi kuwanufaisha makampuni ya simu ambayo kila siku yanazidi kutumaliza sisi watanzania?!!!
  Leo hii Tanzania yenye vyuo vya elimu ya zaidi ya 30 na kila chuo kiatoa kozi tofauti!!!hivi hili jambo kweli ni sawa?mimi nakataa na ninaanza kukosa hata Imani ya hao wasomi walioko hapo TCU,jamani bora hata Ingekuwa kwa Mtandoa ila SMS,hivi kwenye sms kweli utaandika taarifa zako za kutosha?
  uandike jina lako,shule ulizosoma(Olevel and Alevel) ,namba zako za Mitihani na kozi unazoomba na vyuo vyake husika?hivi watanzania ni kweli sisi tuko kwa ajili ya kuboresha au tunataka kuzidi kuharibu!!!!

  Hivi Mlipotaka kuanzisha huo Mfumo je mlikaa na wadau(Vyuo na wanafunzi husika) ili kupata mawazo ni jinsi gani mfanya ili kuboresha huo mfumo?

  Leo hii bodi ya Mikopo ina matatizo mengi sana kwa sababu tu ya wao kujifanya wababe kwa kutoshilikisha wadau na hilo ndo kosa hasa linalozodi kuikwamisha bodi hiyo tegemezi kwa watanzania walio wengi!!!

  TCU kwa hili Mmekurupuka!!!!
   
 4. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Please tell me they are just kidding! I cannot visualize this. Unatuma maombi kwa sms? Tafadhali mwenye kufahamu jinsi utaratibu huu utakavyofanya kazi atusaidie kufafanua hili.
   
Loading...