Maombi ya kujiunga vyuo vikuu sasa kwa 'message'

Maombi ya kujiunga vyuo vikuu sasa kwa 'message'

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,088
Reaction score
165,867
TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imeanzisha mfumo mpya wa wanafunzi kuomba kujiunga na vyuo vikuu ambapo hivi sasa wanafunzi wanatakiwa kuomba kwa kutuma ujumbe kwenda namba 15789 au kutumia mtandao na maombi yote yatapokelewa na TCU.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Mayunga Nkunya, alisema kwa kupitia mfumo huo, waombaji hawatatakiwa kutoa vyeti vya majibu yao wakati wa maombi kwa kuwa TCU itakuwa inayapata moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani nchini( Necta).

Lakini alisema kwa wale wanafunzi watakaoomba kutoka shule za kimataifa watatakiwa kupeleka majibu yao Necta ili yakahakikiwe kabla hawajatuma maombi yao.

``Wanaotakiwa kuomba ni wale waliomaliza kidato cha sita, ndiyo watakaoweza kutumia mfumo huo, na ni kwa kuanzia wale waliomaliza mwaka 1988 hadi leo,``alisema Prof Nkunya na kuongeza;

``Wale ambao hawakumaliza kidato cha tano au wamepitia elimu ya watu wazima hawataweza kutumia mfumo huo kwa kuwa haiwaruhusu,``.

Kuhusu majibu alisema nayo yatatolewa kwa ujumbe mfupi au mtandao na kwamba ni muhimu waombaji wakaambatanisha namba mbili za simu ambazo zinapatikana au email kwaajili ya kurahisisha mambo.

"Ili wanaotaka kutuma maombi waweze kuelewa mfumo huu, TCU imeandaa kitabu chenye maelezo kamili kuhusu namna wanafunzi wanavyoweza kufanya na vitasambazwa katika mikoa yote, kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu, wizarani, Nacte, ofisi za bodi ya mikopo zilizipo mikoani na Dar es Salaam na ofisi za TCU,"alisema.

Profesa Nkunya alisema pia katika tovuti ya TCU, wizara ya elimu, Nacte, vyuo vya elimu ya juu na bodi ya mikopo maelekezo hayo vinapatikana.

Alisema wanafunzi watakaotuma maombi watatakiwa kuomba programu 12 tu kwa taasisi tofauti kama mfumo huo ulivyoandaliwa, lakini katika kufanya hivyo muombaji anatakiwa kuchagua programu nane kwenye taasisi tofauti na programu tatu kwa taasisi moja.

Prof Nkunya alisema mfumo huo unaanza kutumika kuanzia mwaka wa masomo wa 2010/2011 na wanaotuma maombi wanatakiwa kuanza kufanya hivyo kuanzia Februari 15 hadi Mei 31 mwaka huu.

``Hakuna maombi yatakayokubaliwa baada ya mwezi Mei 31 mwaka huu,``alisema Profesa Nkunya.

Alisema waliotuma maombi watapewa majibu yao June 4, na watatakiwa kuhakikisha majibu hayo hadi ifikapo Juni 11 mwaka huu.
Alisema mfumo huo umeigharimu TCU kiasi cha Sh 1 bilioni ambazo zimetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

source : mwananchi website
 
Tanzania kumkucha sasa, sio tna shamba la bibi. Masumbufu yasiyo ya lazima sasa kwa heri!! Labda, tusijipongeze maana wabongo wanaweza kuwa guinea pigs, pengine mfumo huu ukawa mzurim kuusikia lakini ukawa na kero iliyokubuhu.

Leka
 
one big leap, itasaidia kuondoa urasimu, pia udanganyifu wa vyeti feki.
 
mnhhh...i smell rat here....hivi kweli leo tunaomba kujiunga na chuo kikuu kwa just an sms???....sijui jinsi huo mfumo utavyokuwa..ila nahisi tunahitaji kuuchunguza kwa kina.....

tshs 1 billion spent on thisss???????....hapa napo tunahitaji maelezo (we taxpayers)...ndioooo....kwani nini?....na pia hizi sms zinakuwa zinalipiwa...hiyo pesa inakwenda wapi kwa matumizi gani na kwa manufaa ya nani???

ol in ol...kidogo naona tunaanza kujikita kwenye science na technology kwa kiasi flani hiivi....baadae tutasikia mara server imeharibika...mara ohh...wataalamu toka marekani wanataka 2m usd kutengeneza mfumo wa computer ...mara ohhhh...ilimradi kelele tuuuu...ni maoni tuuu
 
Back
Top Bottom