JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
M Chumvi
Mungu ndiye anapanga nani aishi wapi na kwa muda gani, hili linabaki kuwa siri yake.
Wakati mwingine watu hujisahau na kuona maisha anayoishi ni kwa ujanja wake kumbe laaa..
Mamia ya wananchi wa Kiteto Mkoani Manyara, wameshiriki mazishi ya Shekh Mussa Ally Mdugi wa BAKWATA aliyeishi miaka 103 toka azaliwe.
Kwa hesabu za karibu mtu unaweza kusema huyu Shekh ameishi miongo 10 na miaka mitatu au karme moja.
Kwa maisha ya sasa kuishi miaka mingi kiasi hiki no jambo LA kushikuru kwani tumeshuhudia watoto wanaozaliwa na kufa
Shekh Mdugi alikuwa mtu wa watu ambaye hakuwa na makuu, aliona kila MTU ni ndugu yake alithubutu kusema kile anachojua katika kuboresha.
Akisoma wasifu Shekh Mussa Ally Mdugi, Katibu wa BAKWATA Kiteto Shekh Ally Gofah pamoja na mambo mengine alisema Shekh Mdugi alichaguliwa kuwa Shekh wa Wilaya ya Kiteto tar 18/11/1995 na kudumu kwa miaka 23.
Alikuwa kiunganishi cha waislamu na wasio waislamu, alifanya mambo mbalimbali ya kidini ndani na nje ya Wilaya.
Shekh Mussa Ally Mdugi ameacha wajane wanne, watoto kumi na saba, wajukuu 115 na vitukuu 67.
Shekh Juma Mohamed Hincha Makamu Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kiteto àlisema kifo hakizoeleki hivyo amewataka waislamu kuwa na subra.
Akiongea na mamia ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumain Magesa àlisema, marehemu alikidhi haja ya kuwa Kiongozi ndio maana aliongoza kwa miaka 23 akiwa kama kiongozi.
Àlisema marehemu alikuwa mpatanishi wa watu kwani wanasema heri wapatanishi maana hao ni wana wa Mungu
Alisema hitilafu ndani ya jamii lazima atokee hivyo watu kama hao lazima wawepo kwakuwa wanahitajika kwaajili ya kazi hiyo.
Sent using Jamii Forums mobile app