Manyara: Mkuu wa Wilaya asimamia uchomaji moto nyumba Mbulu imo na ya Diwani

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara, Chelestino Mofuga leo amesimamia shughuli ya kuteketezwa kwa moto kwa nyumba sita wilayani humo kwa kukaidi agizo la serikali la kuondoka ndani ya siku saba katika maeneo ya hifadhi.

Miongoni mwa nyumba zilizoteketezwa kwa moto ni pamoja na ya Diwani wa Kata ya Eshkesh, Rumay Ologa ambaye baada ya kupata taarifa hizo alijisalimisha Kituo cha Polisi cha Hydom.

Akizungumza wakati shughuli hiyo ikiendelea, Mofuga amesema njia hiyo itasaidia kulinda hifadhi hiyo.

“Nawataka wavamizi wote wa maeneo ya hifadhi yetu iliyopo Mbulu kuhama kwa hiari yao ndani ya siku saba, kwani taarifa wanazo wanakaidi,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Mofuga amesema operesheni ya kuwaondoa wavamizi hao kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Jeshi la Polisi, watu hao baada ya kuchomewa nyumba zao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kuwapeleka mahakamani.
 
Last edited:
Dah!!! Ila tatizo wengine ukute waliishi hapo toka enzi za mwalimu au before uhuru na mamlaka ziliwaacha
 
Wakenya wanaroho mbaya sana. Mbulu itakua mkoa gani nchini Kenya. Itakua ndaani ndaani huko Kenya.
Tanzania huwezi sikia kitu kama hii. Sana sana utasikia mkuu wa wilaya kawajengea wazee na wasio jiweza Gorofa
 
Back
Top Bottom