JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Benjamin Kuzaga.
Kamanda Kuzaga amesema kiini cha tukio hilo ni ulevi wa mume wa marehemu ambapo alichukua hatua mkononi kwa kumchapa na fimbo na kumsababishia majeraha mwili mwake ikiwemo maumivu katika mguu wake wa Kushoto pamoja na kumvunja mkono wa kushoto.
Marehemu alifikishwa katika kituo cha Afya cha Bashnet kwa ajali ya kupata matibabu na ndipo umauti ulipomkuta.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kusababisha kifo cha mkewe na upelelezi utakapokamilika atafikishwa katika vyombo vya sheria.