Manusura wa shambulio la tindikali: 'Kuna watu wengi wazuri kuliko wabaya'

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Mwanamke wa Ethiopia aliyeshambuliwa kawa tindikali na mumewe mwaka 2017 anasema licha ya hali ngumu anayopitia baada ya shambulio hilo ana kila sababu ya kuwashukuru watu waliomsaidia.

"Kuna watu wengi wazuri duniani kuliko watu wabaya," Atsede Nguse aliaambia BBC kwa njia ya simu kutoka makao yake mapya nchini Marekani.

"Nimeguswa na ukarimu na upendo niliopewa na watu baada ya tukio hilo," mama huyo wa miaka 29 amesema.

Tindikali aliyomwagiwa ilimchoma vibaya na kumharibu uso na na sehemu zingine za mwili wake.

Hakuweza kupata matibabu katika hospitali za Ethiopia na hakuwa na uwezo wa kifedha wa kutafuta matibabu mahali kwengine kokote.

Waliposikia masaibu yaliyomkuta, marafiki zake na wahisani walichangisha fedha za kugharamia matibabu yake nchini Thailand.

Lakini fedha hizo ziliisha kabla ya Bi Atsede kukamilisha matibabu yake hali iliyomfanya kurudi nyumbani akiwa hajapona.

Kwa mara ya pili, mtu mwingine akajitokeza kumsaidia.

'Moyo wangu uliguswa'

Menbere Aklilu, mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake nchini Ethiopia ambaye anaishi Marekani, alisoma kuhusu kisa cha Bi Atsede katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Yeye mwenyewe kama muathirika wa unyanyasaji wa kinyumbani, anasema alitaka kumsaidia.

"Niliposoma kisa chake, nilisikitika sana sawa na watu wengine. Lakini sikutaka yaishie hapo, nilifahamu kuwa ni mama, nikajiuliza: 'Hali ingelikuaje ikiwa mwanangu angelikutwa katika hali ya mtoto wake kwa sasa?'

"Hili liliugusa sana moyo wangu."

Shirika la kimataifa la kuwahudumia manusura wa mashambulio ya tindikali ambalo sio la kiserikali na lenye makao yake nchini Uingereza linakadiria kuwa kati ya wanawake 50 na 75 hushambuliwa kwa tindikali nchini Ethiopia kila mwaka.

Idadi hiyo inaashiria jinsi mzozo wa kinyumbani kiwango ulivyofikia viwango hatari.

Mwaka 2016 ripoti ya serikali ilibainisha kuwa zaidi ya theluthi moja ya wanawake ambao wako katika mahusiano au walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi waliwahi kudhulumiwa kwa njia moja au nyingine kimwili, kingongo au kuhisia mikononi mwa wapenzi wao.

Shambulio dhidi ya Bi Atsede linaweza kutumiwa kama mfano wa kuelezea hali ni mbaya kwa kiasi gani.

Onyo la majirani
Mume wake, aliyemuoa mwaka 2012, angelimpiga wakitofautiana kitu kidogo.

"Majirani zetu walikuwa na hofu, na walikuwa wakinionya kuwa siku moja huenda akaniua. Licha ya hayo yote, niliendelea kuishi naye kwa maslahi ya mtoto wangu. Sikutaka aishi bila malezi ya baba yake, kama nilivyosema."

Hatimaye, mwaka 2015, baada ya kupigwa vibaya hadi meno yake yakang'oka na uso wake kuvimba aliondoka Gambella, magharibi mwa Ethiopia, na kurudi kwao.

"Baada ya kuenda Adigrat, mama yangu na dada yangu wanaoishi Saudi Arabia walinisaidia kuanzisha biashara ndogo ya kuuza manukato. Kwa kweli nilikua nikiendelea vizuri na maisha."

Lakini mwezi Juni mwaka 2017, mume wake alipata nambari yake ya simu, na kuanza kumpigia simu akijidai yuko nje ya nchi.

"Alikuwa akijifanya kama yuko Saudi Arabia. Lakini nikasikia sauti za watoto wakizungumza kwa lugha yetu ya nyumbani, Tigrinya."

Mwezi uliofuata, alikuja hadi nyumbani kwa mama yangu katika kijiji cha Adigrat.

"Alikuwa amejificha [kwenye kichaka karibu na hapo]. Nilimuona akija karibu na mimi. Akanimwagilia kitu kichwani mwangu na mwili wangu mzima," Bi Atsede anakumbuka, jinsi alivyopiga mayowe hadi sauti yake ikapotea.

Tindikali hiyo ilimchoma moja kwa moja.

"Nililia na kuomba msaada. Ndugu zangu walikimbia na kuja kunisaidia. Lakini alitoroka na kuingia kwenyegari lililokuwa likimsubiri."

Bi Atsede aungua vibaya mikono, uso, kifua, masikio, na mguu wake mmoja pia alipoteza uwezo wa kuona.

Hospitali nchini Ethiopia hazikuweza kumsaidia.

Lakini kile kilichomvunja moyo zaidi ni jinsi shambulio hilo lilivyomuathiri mwanawe wa miaka mitano.

"Baada ya shambulio hilo, familia yangu ilimleta mtoto wangu kuja kuniona. Alipoingia katika chumba na kufika mahali nilipokuwa, walimwambia anisalimie, wakisema, 'Ni mama yako.'

"Aliniangalia ana kusema: 'La, huyu sio mama yangu; mama yangu ni mrembo.'"

Baada ya Bi Atsede kurejea nyumbani kutoka Thailand, aliishi katika kituo cha wahanga wa mizozo ya nyumbani mjini Addis Ababa.

Upasuaji wa macho
Bi Menbere alifanikiwa kuwasiliana naye katika kituo hicho, baada ya kupambana na mchakato wa uhamiaji kumwezesha, kumpeleka Marekani.

Alichangisha fedha kwa ushirikiano na marafiki na jamaa zake - na hata watu wasiomjua walijitolea kumsaidia Bi Atsede waliposiki.

1582179690378.png

1582179748028.png
 
Attachments

  • 1582179419374.gif
    1582179419374.gif
    51 bytes · Views: 1
  • 1582179419530.gif
    1582179419530.gif
    51 bytes · Views: 1
  • 1582179419675.gif
    1582179419675.gif
    51 bytes · Views: 1
  • 1582179419855.gif
    1582179419855.gif

View attachment 1363632

View attachment 1363633
Huyo mume wake ana roho ya kishetani sana

BTW,Ipi ni picha yake baada ya kupona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mume fala tu kama ana wivu na sura nzuri ajue wengine wanafata machine sio body

Yote kwa yote yeye ndie kakosa
 
Mapenzi mabaya sana Muogope sana mtu aliyekupenda akapitiliza

Bora hata hawa wanao tucheat cheat,ila ukipata mtu haku cheat,hafanyi ujinga

Kakupenda kaingia mzima mzima,aisee aina hii ya watu wanaopenda hivi ni nusu vichaa

Bora mtu akupende kwa 50% ila hawa wanaotukabidhi mwili,maini,figo,bandama,nk asee

Pona yenu ni msije achana ila mkiachana ni either aliyependa ajidhuru au aliependwa Adhurike.
 
Back
Top Bottom