Manunuzi ya LUKU; Wizi mtupu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manunuzi ya LUKU; Wizi mtupu !

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kudadadeki, Mar 13, 2011.

 1. K

  Kudadadeki Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nilimtuma kijana akanunue LUKU ya Tsh. 12,000/= hapo maeneo ya Science.
  Cha ajabu kaja na Unit 45 tu. Nilipochunguza, nikagundua units hizo chache zimesababishwa na mlundikano wa kodi nilizobebeshwa bila hatia.

  Angalia mlolongo wa kodi hizo;
  1. VAT 18%
  2. EWURA 1%
  3. REA (Rural Electrification Authourity) 3%
  SUB TOTAL; 1,561.57
  4. Municipal Services Tax Invoice 3,340.36

  TOTAL 4,901.93

  Najiuliza,

  1. ni haki katika LUKU ya 12,000/= kupata LUKU ya 7,098/= (59%) ?
  2. ni haki kulipia VAT ? (wakati nimefanya retail business ?)
  3. ni haki kulipia EWURA wakati inapata rudhuku toka Serikali Kuu ?
  4. ni haki kulipia REA wakati wao ni wafanyabiashara wanaosambaza umeme Vijijini ?
  5. kodi chungu nzima ninazolipa katika Manispaa (kodi ya ardhi, kodi ya nyumba etc,etc) hazitoshi hadi waje nikabe koo kwenye umeme ?

  Naomba Ushauri wenu Great Thinkers, tunafanyaje ?......

  Tuwapeleke Mahakamani ? Kuna Wanasheria humu waliotayari kusaidia (Kenya, ningeshapata volunteers Lawyers 200)
   
 2. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  yo' the man, too bad ain't nuh lawyer...this post itself inatosha to fire a complaint, they'll sure have a discomfort explaining all those pointless taxes! Hivi kama unakaa TMK afu ukanua umeme ILALA so hiyo tax ya manispaa/wilaya inaenda wapi?
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Bado Kodi unayokatwa kwenye mshahara wako...kazi kwelikweli.Ningekuwa lawyer ningeshajitolea kukusaidia.
   
 4. w

  warea JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo REA hata sijui inafanya kazi wapi wakati vijijini hakuna umeme!
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Watanzania tunatabia moja. Mtu akikukosea unamsamehe, na kufuta matokeo ya kosa lake. Sidhani hata Mungu anaposamehe makosa yetu hafuta matokeo ya dhambi zetu. Mfano, msichana wa shule akifanya ngono anaweza kumwomba Mungu msamaha na Mungu kwa hakika atamsamehe lakini kama huyo amepata mimba Mungu hatoi ile mimba. Mimba ni matokeo ya dhambi yake. Pia mtu akizini na baadae akamwomba Mungu msamaha kwa hakika Mungu atamsamehe lakini kama huyo mtu atapata ukimwi Mungu hautoi kwani ukimwi ni matokeo ya dhambi. Si kwamba Mungu hajamsamehe bali ni kwa sababu kila kosa linamatokeo yake.
  Hali hii imekuwa ni hulka yetu. Tumezoea kuwasamehi watu na kufuta matokeo ya makosa yao na kwa sababu hiyo wale wanaotuongoza wamejua hivyo kwa hiyo hawana shida. Wanatunga mambo ya kipumbavu halafu tunalalamika tu na hakuna wa kuyafanyia kazi. Hali itaendelea kuwa hivyo kwani kila mtu kasha samehi na kafuta matokeo ya makosa yaliyofanyika.
  Baba wa taifa aliwahi kusema, "Mtu anayekuheshimu akikwambia kitu cha kipumbavu halafu ukakubali, anakudharau." Viongozi wetu wamefanya mambo mengi ya kipumbavu na sisi tunajua ni ya kipumbavu na tumekubaliana nayo sasa wametudharau. Hakuna njia nyingine ya kukwepa hali hii mpka pale tutakaonesha kwamba hatukubaliani na upumbavu wanaotuambia (kutunga). Huo ndo utakuwa mwisho wao kutueleza upumbavu kwani watajua hatutakubaliana.
   
 6. w

  warea JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  EWURA ni idara ya serikali, kwa nini yenyewe inakusanya kodi? Hivi na SUMATRA, TRA, nk nao wana asilimia zao kwenye kodi?
   
 7. N

  Nalonga JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kiongozi nikupe pole kwa kuchelewa kuushtukia huwo wizi mapema!,kwani huo ni wizi mtupu tunaofanyiwa Raia wa Tanzania ndani ya Tanzania.....Ok let us try to close our Eyes and Hears and say....ok with their taxes......then let us ask ourselves "how do we benefit with all thoz crazy taxes??????" with caps NOTHING,NOTHING,NOTHING!.......4 sure something shuld be done to stop this...and i think this is very serious issue that is supposed to be discussed in very broadly ground,and its not politik matter comrade...Now its a CALL for all those patriots Tanzanian lawyers this is your chance to show your patriotism and royality to your poor exploited fellows Tanzanian bana wake up Buddies.
   
Loading...