Manununuzi kupitia AliExpress Application

von tosy

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
251
Reaction score
156
Habari za leo ndugu zangu. Poleni kwa majukumu ya kila siku, naimani mungu yu pamoja nasi katika mihangaiko ya kila siku na kutupatia riziki sisi sote.

Ndugu zangu naomba kufahamishwa kuhusu manunuzi ya bidhaa kupitia application ya AliExpress. Application hii nimeipata nikiwa katika kuangalia bidha mbalimbali mtandaoni. Nimevutiwa na bidhaa zao. Lakini ningependa kupata uzoefu kwa yoyote aliyewahi kufanya order kupitia AliExpress.

Lakini pia jinsi gani naweza kufanya malipo mpaka pale mzigo utakaponifikia. Pia ni njia gani wanayoitumia kufikisha mzigo mana kwenye Application yao nimeona wameandika (free shipingi via China Post Registered Office Mail). Na je kwa waliowahi kutumia njia hii ya manunuzi uhakika wa kupata bidhaa uliyoagiza ni wa kiasi gani.

Ningependa kujua zaidi kwa wale wenye taharifa zaidi juu ya hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati na nitashukuru kwa msaada wenu.
 
Mi mwenyewe Nilitaka Kuanzisha Uzi Kama Huu.. nilishafanya Manunuzi Kwa Njia Ya Ebay nasubiri mzigo na Nikalipa Kwa PAYPAL.. ila Aliexpress hawana Paypal.. Ingawa Ukiangalia Comments za Wanunuzi Nyingi ni Positive

Ngoja tusuburi Wataalam Waje
 
Mimi natumia hii kitu nishafanya order zaid ya mara tatu hivi. Ni very reliable malipo unafanya kupitia atm card yako kama ni visa utajaza details zake. Then unatumiwa unaenda kuchukua pale posta mpya watakutumia sms mzigo ukifika.
 
Kuna Baadhi ya Wauzaji wanatumua AliPay Only..
 
Mi mwenyewe Nilitaka Kuanzisha Uzi Kama Huu.. nilishafanya Manunuzi Kwa Njia Ya Ebay nasubiri mzigo na Nikalipa Kwa PAYPAL.. ila Aliexpress hawana Paypal.. Ingawa Ukiangalia Comments za Wanunuzi Nyingi ni Positive

Ngoja tusuburi Wataalam Waje
Mimi naamini sana kutumia paypal. Kuweka namba zangu za kadi mitandaoni sipati amani japo amazon huwa nanunua kwa kadi na sijawahi pata tatizo
 
Mkuu nitoe tongotongo.... Paypal ni nini na inafanyaje kazi, alipay nayo ipoje cz nmevutiwa sana kutumia hili soko kuhemea bidhaa flani flani... Nielekeze ndugu yangu
 
Mimi natumia hii kitu nishafanya order zaid ya mara tatu hivi. Ni very reliable malipo unafanya kupitia atm card yako kama ni visa utajaza details zake. Then unatumiwa unaenda kuchukua pale posta mpya watakutumia sms mzigo ukifika.
Ulipata bidhaa yako baada ya mida gani mkuu
 
Nimeshafanya order kama 20 kwenye hii site na Visa card ya FNB, hakuna issue na security ya card yako maana unaowapa taarifa ni Aliababa sio wale wauzaji moja kwa moja.

Ukichagua delivery za bei rahisi zote zinakuja kwenye PO Box yako.

Kama ilivyo katika kuagiza kitu chochote kinacholetwa kwa posta/dhl etc kuna chance ndogo ya mzigo kupotea njiani,
mpaka sasa nina package moja ambayo haieleweki iko wapi kati ya order zangu zote, pia hizi njia cheap za delivery zina very basic tracking only sio kama DHL au UPS.
 
Mkuu huo mzigo ambao haueleweki uko wapi, ungeenda pale unapochukulia then wape tracking number. Iliwahi kunitokea onetime, ilipita zaidi ya miezi mitatu sijapokea mesej. Bahati nzuri nilikuwa na packages nyingine ambazo nilipokea mesej. Kufika pale nikamtajia yule mama tracking number ya ule mzigo, nikaupata fresh tu. Muhimu kwenye tracking ya aliexpress ukuonyeshe umefika bongo.
 
Mkuu nitoe tongotongo.... Paypal ni nini na inafanyaje kazi, alipay nayo ipoje cz nmevutiwa sana kutumia hili soko kuhemea bidhaa flani flani... Nielekeze ndugu yangu
Mkuu kuna nyuzi nyingi humu zinazungumzia masuala haya ya paypal na manunuzi mitandaoni yamezungumziwa. Search jinsi ya kufanya manunuzi mtandaoni utaupata uzi ulizungumzia kwa kina sana kila kitu
Pitia uzi huu tulijadili sana Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni
 
Mimi nilikwisha agiza viatu kama majalibio na livipata na malipo nilifanya kwa tigo pesa
 
Kwa mnaoogopa kutumia kadi za bank unaweza kuchukua cash card za visa, hizi zinatolewa na bank za ABC na UBA. Inakuwa ni Visa card ambayo unaijaza hela kiasi unachohitaji, so hata kukitokea tatizo maximum inayoweza kuliwa ni ile balance ya kadi.
 
Habari za leo ndugu zangu. Poleni kwa majukumu ya kila siku, naimani mungu yu pamoja nasi katika mihangaiko ya kila siku na kutupatia riziki sisi sote.

Ndugu zangu naomba kufahamishwa kuhusu manunuzi ya bidhaa kupitia application ya AliExpress. Application hii nimeipata nikiwa katika kuangalia bidha mbalimbali mtandaoni. Nimevutiwa na bidhaa zao. Lakini ningependa kupata uzoefu kwa yoyote aliyewahi kufanya order kupitia AliExpress.

Lakini pia jinsi gani naweza kufanya malipo mpaka pale mzigo utakaponifikia. Pia ni njia gani wanayoitumia kufikisha mzigo mana kwenye Application yao nimeona wameandika (free shipingi via China Post Registered Office Mail). Na je kwa waliowahi kutumia njia hii ya manunuzi uhakika wa kupata bidhaa uliyoagiza ni wa kiasi gani.

Ningependa kujua zaidi kwa wale wenye taharifa zaidi juu ya hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati na nitashukuru kwa msaada wenu.
Na kodi inakuwaje posta ukichukua mzigo?
 
Back
Top Bottom