Manufaa ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami itakayo unganisha Karatu na Mwadui moja kwa moja

z12f

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
638
474
Manufaa ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami itakayo unganisha Karatu na Mwadui moja kwa moja kupitia kaskazini mwa ziwa Eyasi (via Maswa Game reserve).

1) Itaongeza utalii kanda ya ziwa na kanda ya kaskazini. Na kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa kiasi kikubwa.

2) Itaongeza bei ya mazao ya kilimo (na bei ya mifugo) kanda ya ziwa.

3) Itapunguza muda na gharama za usafirishaji kanda ya ziwa. Muda wa safari kutoka Mwanza hadi Arusha utapungua.

4) Itaongeza undugu kati ya kanda ya ziwa na kanda ya kaskazini.

5) Itasaidia watu wa kanda hizo kuwa na exposure zaidi na kupata huduma nzuri zaidi.
Interaction ya wachagga na wasukuma itawasaidia wasukuma wa vijijini kiakili, kwenye mambo ya elimu ya msingi na sekondari, kwenye mambo ya huduma nzuri za mabasi ya usafiri, kwenye mambo ya huduma nzuri za afya (hospitali na pharmacy nzuri), itakua shida kwa wasukuma kutapeliwa mazao yao as wanunuzi wataongezeka kutoka Arusha, Nairobi etc. Wachagga watapata exposure kwenye mambo ya madini (almasi, dhahabu etc) na biashara na nchi za upande ule.

6) Itasaidia biashara kati ya kanda ya kaskazini na kanda ya Ziwa. Pia itaongeza ajira na kujiajiri. In the long run, vijana wengi watapata ajira kwenye sekta ya usafirishaji, maduka, kilimo, mifugo na utalii.

7) Itasaidia sana wasukuma kuendelea, hususan wasukuma wa mkoa wa Simiyu. Kuna miradi michache ya barabara/miundo mbinu ambayo inaweza kuwasaidia wasukuma wa Simiyu zaidi ya mradi huu. Mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Mara na Kigoma nayo itafaidika. Uganda, Rwanda, Burundi na Eastern Congo nao watafaidika.

8) Itachochea ukuaji wa viwanda kwenye kanda hizo mbili.

9) Itakuza uchumi wa Arusha, Moshi, Mwanga, Same na Tanga. Na itasaidia sana wachagga kuendelea. Wachagga wataweza kuuza mazao yao (ndizi, ulezi etc) kwa unafuu huko kanda ya ziwa. Wachagga vile vile watanunua vitu/mazao kwa bei nafuu kutoka kanda ya ziwa. Vijana wakichagga wa vijijini vile vile watanufaika.

10) Itasaidia kanda nyingine za Tanzania kuendelea. Kupanuka kwa uchumi wa kanda ya ziwa kutasababisha watu wa kanda hii kununua bidhaa za viwanda (cement etc) na mazao mbali mbali kutoka maeneo mengine ya Tanzania e.g. Dsm, Dodoma, Mbeya, Lindi/Mtwara, Ruvuma etc.

NB: Kutokana na ufinyu wa bajeti, tunaweza tukaanza na barabara ya vumbi halafu baadae tuka upgrade ikawa ya lami.

Update

Nimecheki ramani, yes ni kweli, barabara za vumbi zipo. Kuna barabara ya vumbi inatoka mji wa Ngorongoro inapitia Kakesio then Banyu (in Maswa Game Reserve) then Banyu tena (after Maswa Game reserve) then Lalago (karibia na Mwadui; kwenye main road ya Mwanza na Musoma). Hii ndio barabara ambayo nashauri ni vizuri ikawekewa lami hivi karibuni, ili itumiwe na watalii na magari madogo binafsi. Barabara hii ni vizuri itumike wakati kuna mwanga wa jua, isitumike usiku. This road is approximately 180 kms.

Baadae barabara ya Seronera, Ruhoga, Nata, Mugela mpaka njia ya Ushashi-Musoma nayo inaweza kuwekewa lami. Ili pia itumike na watalii na magari madogo binafsi. Hii barabara inapitia ndani ya Serengeti National Park na Grumeti Game Reserve. Barabara hii pia ni vizuri itumike wakati kuna mwanga wa jua, isitumike usiku.

Kuna mdau ambae ame elezea kwa urefu na kina, debate ya commercial highway.

Baadae kama kuna mipango ya kujenga commercial highway, ni vizuri commercial highway hiyo ikapitia kusini mwa ziwa Eyasi (nje ya eneo la hifadhi).
 
Labda na wataalamu wa barabara wanaweza kukubaliana na hoja hii
 
Inaanza kujengwa lini? Halafu umerudia rudia sana. Hoja moja inakuwa na pointi kumi za nini? Ungetulia ungeiweka vizuri sana
 
Umeifinya sana hii habari maana ni kama umetoa suggestions tu kwa kuanza na barabara za vumbi angali zipo sema si za kupita magari makubwa kwa kuwa ni sehemu zenye tope sana....

Ila serikali inampango huo sema sijui utaanza lini japo baadhi ya maeneo kama wilaya ya meatu tunaona watu wa tanroad wanapima kila siku....
 
Nimecheki ramani, yes ni kweli, barabara za vumbi zipo. Kuna barabara ya vumbi inatoka mji wa Ngorongoro inapitia Kakesio then Banyu (in Maswa Game Reserve) then Banyu tena (after Maswa Game reserve) then Lalago (karibia na Mwadui; kwenye main road ya Mwanza na Musoma). Hii ndio barabara ambayo nashauri ni vizuri ikawekewa lami hivi karibuni, ili itumiwe na watalii na magari madogo binafsi. Barabara hii ni vizuri itumike wakati kuna mwanga wa jua, isitumike usiku. This road is approximately 180 kms.

Baadae barabara ya Seronera, Ruhoga, Nata, Mugela mpaka njia ya Ushashi-Musoma nayo inaweza kuwekewa lami. Ili pia itumike na watalii na magari madogo binafsi. Hii barabara inapitia ndani ya Serengeti National Park na Grumeti Game Reserve. Barabara hii pia ni vizuri itumike wakati kuna mwanga wa jua, isitumike usiku.

Kuna mdau ambae ame elezea kwa urefu na kina, debate ya commercial highway.

Baadae kama kuna mipango ya kujenga commercial highway, ni vizuri commercial highway hiyo ikapitia kusini mwa ziwa Eyasi (nje ya eneo la hifadhi).
 
Nimecheki ramani, yes ni kweli, barabara za vumbi zipo. Kuna barabara ya vumbi inatoka mji wa Ngorongoro inapitia Kakesio then Banyu (in Maswa Game Reserve) then Banyu tena (after Maswa Game reserve) then Lalago (karibia na Mwadui; kwenye main road ya Mwanza na Musoma). Hii ndio barabara ambayo nashauri ni vizuri ikawekewa lami hivi karibuni, ili itumiwe na watalii na magari madogo binafsi. Barabara hii ni vizuri itumike wakati kuna mwanga wa jua, isitumike usiku.

Baadae barabara ya Seronera, Ruhoga, Nata, Mugela mpaka njia ya Ushashi-Musoma nayo inaweza kuwekewa lami. Ili pia itumike na watalii na magari madogo binafsi. Hii barabara inapitia ndani ya Serengeti National Park na Grumeti Game Reserve. Barabara hii pia ni vizuri itumike wakati kuna mwanga wa jua, isitumike usiku.

Kuna mdau ambae ame elezea kwa urefu na kina, debate ya commercial highway.

Baadae kama kuna mipango ya kujenga commercial highway, ni vizuri commercial highway hiyo ikapitia kusini mwa ziwa Eyasi (nje ya eneo la hifadhi).
mkuu nakumbuka kama mwezi uliopita nadhani,nilisikia katika kikao cha bodi ya barabara mkoa wa shinyanga meneja wa tanroad alisema usanifu wa barabara ya kolandoto-karatu kupitia kusini(?)mwa ziwa eyasi kwa kiwango cha rami umekamilika sasa inatafutwa pesa itakayowezesha ujenzi kuanza.Nadhan mkuu unaongelea hii barabara.
 
Back
Top Bottom