py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,476
- 4,447
Misimu kadhaa nyuma kabla ya Ko Deuji kujingiza klabuni simba timu hii inayopatikana mitaa ya msimbazi ilikuwa inasajili wachezaji kwa mafungu mafungu na ilikuwa inapata shida sana kusajili wachezaji waliokuwa wanawaniwa na yanga.Nani anasahau ishu ya mbuyu Twite nk pia wachezaji walikuwa wanaondoka kwa kisingizio cha kutolipwa mishahara kama Singano nk pia wachezaji walikuwa wanalalamika mara kwa Mara kucheleweshewa mishahara hivyo walikuwa wanatingisha viberiti huku yanga wakijinasibu wakimataifa ,wanayo pesa
Mwaka Jana ulikuwa neema kwa simba baada ya mfanyabiashara Mo Deuji kutaka kununua share klabu hapo hivyo amekuwa akisaidia kutoa pesa ya kusajili wachezaji, kulipa mishahara wachezaji kwa wakati huku akisubiria mchakato wa mabadiliko ufanyike simba leo hii inayo jeuri.
Tukirudi yanga ase hawa jamaa wanapitia kipindi kigumu hivi sasa baada ya mwenyekiti wao Yusuf Kanji kujiuzuru.Leo hii yanga inapigwa bao na Azam kwenye usajili wa mchezaji waziri junior ,huyu junior alisema yanga walikuwa wanasuasua pesa hawana ndio maana Azam walivyomfuata fasta akamwaga wino.pia mchezaji wa Mbao fc Buswita alikuwa anawaniwa na yanga na ilijulikana wazi atamwaga wino jangwani lakini sababu ya ukata simba ikaingilia dili na kuwafanyia umafia yanga na saizi fundi huyu ametia saini msimbazi.
Kiungo fundi mjanja mjanja mzaliwa wa Gisenyi mzee wa pasi mnato ,pasi mnyoofu ,pasi za nyoka Haruna fadhil hakizimana Niyonzima yupo kwenye hatua za mwisho kujiunga na simba ,Kwa takriban miezi kadhaa niyonzima hajalipwa stahiki zake na simba wanajiandaa kumwaga pesa za usajili
Zile jeuri za yanga za kufanya umafia Twite ,kaseke ,kessy nk zipo wapi
Licha ya yanga kuingia ubia na sports pesa kama vile simba lakini inaonyesha bado mambo sio mazuri.
Wakati simba wanaanza kuneemeka na mabillioni ya Mo Deuji huku kwa yanga wanashangaa shangaa na miayo ya Mkemi na Mzee Akili Mali .
Manji alishutumiwa kuwa ana miliki pasi ya kusafiria ya nchi 2 hivyo serikali ikaamua kuzuia accounts zake,tokea accounts za Manji zizuiliwe na idara ya uhamiaji klabu ya yanga imekuwa ikipitia wakati mgumu.
Lakini baada ya accounts za Manji kuachiwa/kufunguliwa ameonekana mnyonge na kuandika barua ya kujiuzuru akidai afya yake haipo vizuri na ameshauriwa na tabibu wake apumzike.Na ikumbukwe kuna watu walikuwa wanampiga vijembe kila kukicha aiachie yanga sababu ni kama amejimilikisha.
Zile jeuri za yanga zipo wapi yaani leo hii simba inayo jeuri ya kumng'oa Niyonzima yanga ?
Leo hii simba inawafanyia umafia yanga kwenye usajili
Zile 5 naona zitajirudia ase