Manji apewa saa 48 kuhama Quality Plaza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji apewa saa 48 kuhama Quality Plaza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MFANYABIASHA maarufu nchini Yusuf Manji, amepewa notisi ya saa 48 na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), kuhama katika jengo la Quality Plaza Complex.

  Jengo hilo ambalo liko kitalu namba 182/2 barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam ni mali ya PSPF na Manji ambaye ni mpangaji anadaiwa kukiuka masharti ya mkataba wa upangishwaji kwa kushindwa kulipa kodi.

  Wakili wa PSPF, Benitho Mandele, alisema katika barua yake yenye kumbukumbu namba DLA/IMAGE/2010/12 kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Quality Group Limited, Manji anadaiwa kodi ya kuanzia Aprili, 2009 hadi Desemba 2010, hivyo jumla ya deni lote ni dola 2,335,189.06 za Marekani.

  “Manji, ameshindwa kuheshimu makubaliano baina ya wateja wangu ambao ni PSPF na yeye… tangu Aprili mwaka jana hadi Desemba, 2010 ameshindwa kulipa kodi.

  “Tumempa masaa 48 kuanzia leo hadi kesho kutwa awe amehama katika jengo lile,” alisema wakili huyo wa PSPF.

  Alisema kwa kutambua uzito wa suala hilo amemwandikia Manji barua ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake kwenda kwa Mkurugenzi wa Quality Group Limited, Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.

  Kwa mujibu wa barua hiyo, Manji amepewa nakala ya barua hiyo kama Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Quality Group Limited.

  Hata hivyo, Manji alipotafutwa na gazeti hili kwa njia ya simu yake ya mkononi, alikata simu baada ya kuulizwa kama amepata barua hiyo.

  Hata hivyo, baadaye gazeti hili lilipomtafuta kupitia simu yake hiyo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni katibu mukhtasi ambaye alisema ujumbe umefika.

  Hadi tunakwenda mitamboni jana jioni kulikuwa hakuna majibu yoyote kutoka kwake.
   
Loading...