Manji aanika siri ya uuzwaji wa UDA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji aanika siri ya uuzwaji wa UDA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 10, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  IJUMAA, 09 MACHI 2012 06:10 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM


  [​IMG]Moja ya mabasi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA)  SAKATA la uuzwaji wa Shirika la Usafirishaji la mkoa wa Dar es Salaam (UDA), limechukua sura mpya baada ya Mwenyekiti wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuf Manji, kuibuka na kukana hatua za kutaka kununua kampuni hiyo kinyemela.
  Hatau hiyo ya Manji, imekuja siku moja baada ya kudaiwa na kufadhli harakati za kutaka kuing'oa kampuni ya Simon Group katika umiliki wa UDA.

  Kwa mujibu wa taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Manji alisema hausiki na harakati za viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika sakata la kuing'oa Kampuni hiyo kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

  "Mwalimu Nyerere, aliwahi kutuonya kwamba uongo ukiachiwa kuendelea kwa muda mrefu, unageuka kuwa ukweli na watu wanauamini, nilidaiwa kuwatumia Wenyeviti wawili wa Kamati za Bunge ili kufanikisha hilo ambao ni Dk. Abdallah Kigoda na Zitto Kabwe ili kulipata Shirika hili kwa mlango wa nyuma. Hivyo nimeonelea kutoendelea kukaa kimya wakati Taifa linapotoshwa.

  "Ni ukweli ulio wazi mimi kama Kiongozi wa Quality Group, baada ya kusikia minong'ono na taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba UDA limebinafsishwa kwa Simon Group, niliamua kuwaandikia barua wenyeviti hao wa Kamati mbili za Bunge ambazo ndizo zenye jukumu la uangalizi wa mashirika ya umma.

  "Lengo kubwa la kuandika barua hizo ni kuweza kuomba kupata ufafanuzi juu ya taratibu zilizotumika kulibinafsisha shirika hilo, niliwaeleza kwa kinagaubaga kwamba nimesikia kupitia vyombo vya habari kuwa uuzwaji wa hisa asimilia 51 za UDA umefanywa, na tayari Kampuni ya Simon Group imepewa," alisema Manji, katika taarifa yake.

  Katika Barua hiyo Manji alikiri kushiriki katika tenda mbili za UDA ambapo ya kwanza ilifanyika mwaka 2005, ka kuzishirikisha kampuni tatu huku nyingine ikirudiwa tena mwaka 2007 ambapo kampuni ya Quality Group pekee ndiyo ilishiriki.

  Barua hiyo kwenda kwa wenyeviti wa Kamati hizo za Bunge ya Agosti 14, iliambatanishwa vivuli vya nyaraka za tenda hiyo na kutumwa kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PPSRFC.

  "Katika tenda ya mwaka 2007, tulieleza kuwa tuko tayari kuingia ubia wa shirika hilo kwa gharama ya Sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa hisa 49 za UDA.

  "Na kama tungefanikiwa kupata tenda hiyo nilieleza wazi tungewekeza Dola za Marekani milioni 10, kwa ajili ya ukarabati wa karakana. Pia tulieleza kuwa tungeleta mabasi 150 chini ya utaratibu wa DART.

  "Tulifanya hivyo tukizingatia ukweli kwamba tulikuwa na uzoefu wa miaka 30 katika sekta ya usafirishaji nchini kwa kushirikiana na makampuni makubwa ya usafirishaji na usafiti duniani kama vile Honda, ISUZU na Bridgestone, na tuliomba tenda hiyo tukiwa tayari na makubaliano na kampuni ya Hess kutoka Swatzerland," alisema Manji

  Mwisho

   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  mambo mengine bwana, kwani Manji ni mwanasiasa ama issue hii ni ya kisiasa? sio mambo ya Business kweli? hebu ipeleke huko basi ama ipeleke kwenye jukwaa la habari mchanganyiko. Hapa acha tumjadili Malima waziri aliyeibiwa na changudoa
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  sasa kwa nini manji alinyimwa hiyo tenda kama kampuni lake lilikuwa na vision nzuri hivi?
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  twenzetu kumjadili malima aliyelizwa na CD
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mwana Mpotevu!
  Kwanza karibu sana baada kupote mda kidogo hapa jamvini...
  Ila leo naona una makusudi na mbavu zangu, kila ninapoikuta post yako unanichekesha sana...
  Nadhani ukirudi jamvini kukipambazuka utakuwa na data za kutosha kuhusu huyo waziri mwenye "vijipesa"
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Haujui Manji aligombea Ubunge wa Kigamboni - kwahiyo ni Mwanasiasa
   
 7. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Manji amuombe kwa umma unaomheshimu mwalimu Nyerere kwa kumtumia kuhalalisha upuuzi wake. Kitendo cha Mangi kumnukuu Nyerere ni sawa na shetani kumnukuu Yesu hata Mohammad. Kwani anadhani kuwa watanzania hawajui kuwa yeye ni kibaka kama Rostam? Go to hell Manji na rongorongo zako.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe kwani Nyerere ni nani hata asinukuliwe? huyo Nyerere alikuwa ni Rais wa baadhi tu ya Watanzania? hata wengine wasiweze kumnukuu? kumfananisha Nyerere na Yesu (AS) au Muhammad (SAW) ni ujinga wa hali ya juu.

  Na huyo Manji alikubakia nani wako hata umuite hivyo, labda kuna siri kati yako na yake hatuijui?

  Hiyo UDA kama huelewi, basi zake 90% zimetengenezwa bodi zake na kina manji wa Quality Body toka wakati wa Nyerere. Huo ukoo hata Nyerere anaujuwa na haukutaifishiwa mali zake na Nyerere, jiulize kwanini?
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hiyo bilion 1.5 si ni pesa tu ya kununua kiwanja kariakoo sasa UDA ina rasilimali ngapi< viwanja na karakana kibao yani hisa za 49% anunue kwa 1.5bil huu ni upuuzi wa karne
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  watakwambia kwa sababu mhindi si unajua idd simba na sera yake ya uzawa pori
   
 11. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo la viongozi wetu wanapenda vitu visivyo dhahiri,waliona Manji akipewa mradi huo utakuwa
  endelevu na wao hawatapata kuendelea kufyonza humo.Lakini ukweli mnyonge mnyongeni haki
  yake mpeni, kwa Vision hizi za Manji suala la usafiri ktk jiji la Dar-es-salaam lingekuwa historia.
   
Loading...