Manispaa za Dar es salaam wekeni vyoo vya kulipia kwenye public beach

boyson onlye

JF-Expert Member
Sep 13, 2015
1,108
1,397
Habari jf

Naomba mamlaka husika waliangalie jambo hili kwa jicho la tatu, kuna kampeni zinafanyika za usafi sawa zimepokelewa vizuri na naona mmeweka dust bean nyingi kwenye barabara za maeneo ya osterbay jiji hapa, nawapongeza kwa jambo hili ni hatua Nzuri


Sasa tuje kwenye hili beach kama coco, kawe na beach nyingine ambazo watu wengi wanapenda kwenda siku za weak end na sikukuu, hivi mshawai kujiuliza hawa watu wanapeleka wapi mikojo Yao na kinyesi, hasa coco mihogo vipi watu wakishakula wakashiba wakitaka kwenda haja wanafanyaje,

Nashauri manispaa husika zianzishe miradi ya public toilet ili kujiongezea kipato na kuweka mazingira safi, hizi elfu 50 mnazotutoza mkitukuta tunajisaidia polini ni uonevu mnataka tupeleke wapi mikojo na kinyesi wakati beach hazina vyoo na sisi tushakula mihogo tumeshiba

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom