Manispaa ya Ubungo yaomba radhi kwa mishahara kuchelewa katika Hospitali ya Sinza Palestina

Manispaa ya Ubungo yaomba radhi kwa mishahara kuchelewa katika Hospitali ya Sinza Palestina

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
TAARIFA KWA UMMA@jamiiforums.webp
TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MALALAMIKO YA UCHELEWESHAJI WA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA MIKATABA KUPITIA MTANDAO WA JAMII FORUM TAREHE 08/03/2026

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inapenda kuufahamisha umma kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa na watumishi wa mikataba wa hospitali ya Sinza Palestina yanayohusu ucheleweshaji wa malipo ya mishahara yao kupitia mtandao wa kijamii wa Jamii Forum tarehe 08 Machi, 2026.

Hoja ya awali ~ Watumishi wa Mkataba Hospitali ya Sinza Palestina tunacheleweshewa mishahara, kila tukiuliza wanasema “Next week”

Halmashauri inakiri kuwepo kwa changamoto ya ucheleweshaji wa malipo ya mishahara kwa watumishi hao, hali iliyotokana na hitilafu za kiufundi katika mfumo wa ulipaji wa fedha. Hitilafu hizo ziliathiri mifumo ya ulipaji kwa kipindi cha takribani wiki moja, hali iliyopelekea kuchelewa kufanya malipo kwa wakati huku mchakato wa malipo kwa ngazi mbalimbali ulikuwa ukiendelea.

Hata hivyo, Halmashauri inapenda kuujulisha umma kuwa changamoto hizo za mifumo zimeshatatuliwa, na mpaka kufikia leo jumatatu machi 09, 2026, watumishi wote wa hospitali ya Sinza Palestina wameshalipwa mishahara yao ya mwezi Februari. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inawaomba radhi watumishi wote wa hospitali hiyo kwa changamoto zilizojitokeza.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
 
Jamii forum imekuwa RELIABLE kuliko main stream media nyingi...
Godbless JAMII FORUM,wamesikika,wamejibiwa!
 
Back
Top Bottom