Responded Manispaa ya Ubungo: Malipo ya mshahara wa madereva yamechelewa kutokana na hitilafu za kiufundi katika mifumo ya ulipaji wa fedha

Responded Manispaa ya Ubungo: Malipo ya mshahara wa madereva yamechelewa kutokana na hitilafu za kiufundi katika mifumo ya ulipaji wa fedha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
TAARIFA YA UFANUZI KUHUSU MALALAMIKO YA UCHELEWESHAJI WA MISHAHARA KWA MADEREVA WA MIKATABA – HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII WA JAMII FORUM TAREHE 10.02.2026

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inapenda kuufahamisha umma kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa na madereva wa mikataba yanayohusu ucheleweshaji wa malipo ya mishahara yao kupitia mtandao wa kijamii wa “JamiiForums tarehe 10 Februari, 2026”.

Kusoma hoja ya awali, bofya hapa ~ Madereva wa mkataba Ubungo halmashauri tunacheleweshwa mishahara

Halmashauri inakiri kuwepo kwa changamoto ya ucheleweshaji wa malipo ya mishahara kwa madereva hao, hali iliyotokana na hitilafu za kiufundi katika mifumo ya ulipaji wa fedha. Hitilafu hizo ziliathiri mifumo ya malipo kwa kipindi cha takribani wiki mbili, na kusababisha kushindwa kutekeleza malipo kwa wakati uliopangwa.

Hata hivyo, Halmashauri inapenda kuujulisha umma kuwa changamoto hizo za mifumo zimeshatatuliwa, na kwa sasa mchakato wa ulipaji wa mishahara unaendelea. Madereva wote walioathirika watalipwa stahiki zao muda wowote kuanzia sasa

Imetolewa na
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
 
Back
Top Bottom