Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kutoa wito kwa Serikali kuingilia kati suala la Kampuni inayohusika na kukamata wanaoegesha vibaya vyombo vya usafiri vya moto (wrong parking), akidai huduma zao sio nzuri na pia Faini ya Tsh. 80,000 haendani na kosa, ufafanuzi umetolewa na Mamlaka husika.
Mdau huyo alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikamata magari hata kama yamegaguliwa (scanned) na wanaokusanya fedha za kuegesha magari na hata kukamata vyombo vilivyoegesha kwa dharura.
Kusoma zaidi alichoeleza Mwanachi bofya hapa ~ Kuna Kampuni inakamata magari kwa uonevu kwa kisingizio cha kuegesha vibaya Ubungo
Huu hapa ufafanuzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo...
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU MALALAMIKO YA MWANANCHI KUHUSIANA NA UKAMATAJI WA MAEGESHO YASIYO RASIMI (WRONG PARKING)
1. Utangulizi
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepokea malalamiko ya wananchi yaliyochapishwa katika jukwaa la JamiiAfrica na mtandao wao wa Instagram wa JamiiForums yenye Kichwa cha Habari kisemacho "Kuna Kampuni Ubungo inakamata Magari kwa uonevu kwa kisingizio cha kuegesha vibaya" huku ikisema imekuwa ikikamata magari licha ya magari hayo kuwa tayari yamekaguliwa na wakati mwingine wanakamata pale ambapo dereva amesimama kwa dharura.
Boss Kazi Ltd, ni wakala aliyepewa rasmi jukumu la kusimamia na kukusanya faini za maegesho kinyume cha utaratibu (wrong parking) kupitia mkataba ulioanza kutekelezwa tarehe 14 Aprili 2025.
Malalamiko yaliyochapishwa na Bw. Venance Tarimo kupitia JamiiAfrica, alieleza kutoridhishwa na namna maafisa walivyoshughulikia suala lake tarehe 16 Agosti 2025, baada ya gari lake kukutwa limeegeshwa kinyume na taratibu.
2. Ukweli Kuhusu Tukio
Ni kweli kuwa gari la Bw. Tarimo lilibainika kuwa limepaki sehemu isiyoruhusiwa. Alielezwa kuhusu kosa hilo na kupewa fomu rasmi inayobainisha kosa pamoja na kupewa namba ya malipo (Control number) juu ya fomu hiyo ambayo ni 992060420258 ambayo alilipa. Hata hivyo, kutokana na changamoto za kimtandao zilizokuwepo, alihisi anatengenezewa mazingira ya kutoa pesa taslimu- jambo ambalo tunalichukulia kwa uzito na tunaendelea kulifuatilia.
3. Utaratibu Rasmi wa Kukamata na Malipo
Kwa mujibu wa mkataba na wakala wetu, wakaguzi wa maegesho kinyume cha utaratibu (wrong parking):
Wanatumia vitambulisho halali.
Hukamata magari yaliyopaki kinyume na maeneo rasmi ya maegesho.
Wanapobaini kosa, wanampatia mmiliki wa gari fomu ya kosa yenye maelezo ya makosa na kiwango cha faini.
Control number huandikwa juu ya fomu hiyo, na mwananchi anaelekezwa kulipa kupitia: Mfumo wa malipo ya kielektroniki (control number) au kupitia POS machine rasmi na unapewa Risiti kuthibitisha kuwa umekamilisha malipo.
Kiwango halali cha faini kwa kosa la wrong parking ni Shilingi 80,000 pekee, na hakipaswi kuzidi hapo kwa hali yoyote. Hakuna malipo ya papo kwa hapo yanayoruhusiwa nje ya mifumo hii. Na hii ni kwa maeneo yote ndani ya Manispaa ya Ubungo ikiwemo Soko la Mbezi Shule na Soko Mabibo ambapo malalamiko kama haya yametolewa.
4. Wanaokaguliwa (Kuskaniwa) kwenye Maegesho/Parking
Ni muhimu kueleza kwamba magari yanayopaki katika maeneo sahihi ya maegesho, lakini bado yanakaguliwa au kuskaniwa kwa ajili ya uthibitisho wa uhalali wa maegesho, hawatozwi faini wala kulazimishwa kulipa papo kwa papo. Lengo ni kuhakikisha kuwa huduma inatekelezwa kwa haki na kwa kuzingatia ushahidi.
5. Tofauti ya Utaratibu wa Halmashauri na Jeshi la Polisi
Tunatambua kuwepo kwa sintofahamu miongoni mwa wananchi kuhusu utaratibu wa faini za Maegesho. Utaratibu unaotumika na Halmashauri kupitia wakala wetu (Boss Kazi Ltd) ni tofauti na ule wa Jeshi la Polisi:
Halmashauri: Mwananchi aliyekutwa na kosa hupewa Namba ya malipo (control number) na hataruhusiwa kuondoka hadi awe amelipa faini husika.
Polisi: Mara nyingi hukamata gari au dereva, na kutoa faini ambayo inaweza kulipwa baada ya kuondoka eneo la tukio.
Tunaomba wananchi wafahamu tofauti hii ya kiutendaji ili kuepuka mkanganyiko au dhana potofu.
6. Maelekezo kwa Watendaji wa Boss Kazi Ltd
Pamoja na kuendelea na kazi ya kukusanya ushuru, Mzabuni na watendaji wake wamesisitizwa:
Kufanya kazi kwa kufuata masharti ya mkataba na sheria za nchi.
Kuwahudumia wananchi kwa staha, heshima na weledi.
Kupiga picha au kuchukua ushahidi wa makosa kabla ya kutoa faini ili kuepusha sintofahamu.
Kutoa elimu ya kutosha kwa kila mwananchi anayekamatwa, kuhusu kosa lake na namna ya kulipa.
7. Ukipata changamoto Barabarani:
Kama ni dharura ya Muda mrefu, Mfano gari limezimika weka alama zinazokubalika kuonyesha kuwa kuna dharura iliyokupata.
Ikiwa ni dharura ya Muda mfupi, Mfano unamsubiri mtu, washa taa za tahadhali (Double Hazard) au peleka kwenye maegesho rasmi.
8. Wito kwa Wananchi
Endapo kuna mwananchi yeyote ambaye hajaridhika na namna tukio lake lilivyoshughulikiwa, anakaribishwa kufika ofisi ya MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yake rasmi. Tunayo dhamira ya kushughulikia kila hoja kwa haki, weledi wakati wote.
Tunasisitiza kuwa lengo letu ni kutekeleza jukumu hili kwa uwazi, weledi na kwa kuzingatia haki za kila mwananchi. Ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kuhakikisha miji yetu inakuwa safi, salama na yenye mpangilio bora wa maegesho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Pia soma:
~ Malipo ya maegesho ya SGR kwanini yasilipwe kwa control number? Huu mradi una mkono wa nani?
~ Changamoto za Ufuatiliaji wa Magari na Utoaji wa Faini Katika Maeneo ya Mlimani City na Survey Road kwa madai ya maegesho yasiyo rasmi (Wrong parking)
~ Chalamila: Zile Kampuni za kukamata "Wrong Parking" lile ni genge la rushwa