Manispaa ya Tabora tabaani

wadabali

Member
Jan 20, 2013
9
1
Ndugu watanzania wenzangu kwa muda mrefu nimefanya utafiti kuhusu uendeshaji wa halmashauri zetu hasa kupitia manispaa ya Tabora ambayo ina jumla ya kata ishirini na tano japo kutokana upeo mdogo wa madiwani wetu wanampango wa kugawa kata zaidi ya tano lakini kata zilizpo kwa majina ni kama zifuatazo.

MTENDENI,IFUCHA,TUMBI,MALOLO,MISHA,KABILA,IKOMWA,KAKOLA,UYUI,KILOLENI,TAMBUKARELI,CHEMCHEM,NG'AMBO,
KITETE,CHEYO,ITETEMIA,KALUNDE,ITONJANDA,IPULI,ISEVYA,MTAKUJA,GONGONI,KANYENYE na NDEVELWA kutokana na uchunguzi wangu nimebaini yafuatayo

1 Baraza la madiwani ni dhaifu kupita maelezo kupitia mijadala,maazimio na kamati zake

2Meya ,Ndugu Gulamwa na Naibu wake ,Ndugu waziri hawana uwezo wa kuendesha halmashauri na elimu zao zina mashaka.

3 Mfuko wa jimbo umeishia mikononi mwa mbunge,Range na anaowajua

4 Miradi ya maendeleo haitekelezwi kwa ufasaha hata ikitekelezwa ipo chini ya kiwango mfano maji,afya,kilimo,elimu n.k.

5 Ufisadi ambao umeanishwa kwenye ripoti ya mkaguzi wa ndani ambayo imeguza katika maeneo yafuatayo kugushi safari,idara ya ardhi,mishahara hewa watumishi 503,na uchakajuaji wa miradi ya maendeleo.

6 Halmashauri ina kesi zaidi ya ishirini mahakamani ambaza zaidi ya asilimia tisi na nane ,halmashauri inadiwa na hakuna kesi hata moja ambayo imesikilizwa kutokana na uzembe wao.

7 Usafi limekuwa janga na sugu kwa inayoitwa manispaa.

Mwisho nimefanya ziara katika kata ya Kakola ambayo ni km 17 kutoka mjini hapa nimesikitishwa na jambo moja hakuna hata kisima cha maji badala yake wanachota kwenye dibwi ambalao huingiza maji machafu ya mvua na pia hutumika na mifugo kwa kuwa maisha ya wananchi 2033 takwimu ambazo zimebandikwa kwenye ofisi ya mtendaji wa kata yapo hatarini TAMKO tunaipa halmashauri siku 60 vinginevyo nguvu ya umma itachukua mkondo wake, pia madiwani na viongozi wa kata na vijiji itisheni mikutano ya wananchi kuwasomea mapato na matumizi kila baaba ya miezi mitatu kama sheria inavyoagiza.

KUANZIA LEO MIMI SAUTI YA MKOA WA TABORA MPAKA KIELEWEKE NAOMBA USHIRIKINO KWA WOTE WAPENDA MABADILIKO
 
Huu mkoa kwa kweli inasikitisha sana. Wanyamwezi wengi wamesoma lakini wanaishi Dar na maeneo mengine mazuri ya nchi hata mbunge wao wa zamani (Marehemu) amezikwa Dar hivi tu majuzi. Mkoa hauna mwamko na elimu ndo hiyo ilifariki na JK Nyerere pamoja. Nakupongeza sana kaka kama utakuwa mmoja ya wale waliotoka usingizini ila wanyamwezi kwa kweli mnastaili kupigwa viboko huko mliko kwa kusahau nyumbani kwenu.
 
Back
Top Bottom