Manispaa ya morogoro yapigwa stop

zilzal

Senior Member
Jul 6, 2008
136
26
Taarifa iliyopatikana ni kwamba,wafanyabiashara wa Nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Morogoro wamefanikiwa kupata Amri ya muda ya mahakama inayowasimamisha BAMM Solutions na Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro kuendelea kukusanya ushuru wa mahoteli"hotel levy" baada ya kubainika kuwa sheria ya ushuru wa mahoteli (Hotels Act cap. 105) ambayo walikuwa wanaendelea kuitumia ilikuwa imeshafutwa kwa sheria mpya ya utalii ( Tourism Act.no.29 of 2008) ilivoanza kutumika mwezi wa Aprili,2009.Uamuzi huo umeleta mtafaruku mkubwa baina ya Ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa na kampuni ya BAMMS Solutions.
 
Back
Top Bottom