Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Kumekuwa na tabia iliyozoeleka kwa viongozi wa Manispaa ya Temeke na ofisi ya utamaduni chini ya Mkuu wa wilaya Temeke kutoa vibali vya sherehe zinazoambatana na kupiga muziki ktk makazi ya watu usiku na hivyo kusababisha kero na usumbufu kwa watu kushindwa kulala.
Tabia hii pamoja na kwamba inakiuka sheria lakini wahusika wameziba pamba masikioni kwa kuwa wananufaika kwa rushwa ktk upatikanaji wa vibali hivyo.
Eneo linaloonekana kuathirika na vibali hivi ni pamoja na mbagala, kiburugwa, na maeneo mengine yanayozunguka maeneo haya.
Kwa kuwa sheria inakataza na wahusika wanatoa vibali huku wakijua kuwa ni kosa tunakusudia sasa kila mahali kitakapotolewa kibali cha aina hii tumpelekee mhe. Waziri mkuu ili hatua zichukuliwe.
Haiingii akilini mkuu wa wilaya yupo, afisa tawala yupo na mkurugenzi wa manispaa wote washindwe kudhibiti watendaji wao juu ya jambo hili.
Hatuwezi kuendelea kuishi chini ya watu wanaofanya kazi kwa mazoea bila kufuata taratibu za nchi tulizojiwekea. Kiongozi yeyote atakayeidhinisha kibali kitakacholeta usumbufu kwa wananchi usiku bila yeye kujiridhisha juu ya matumizi yake tutalala naye mbele. Tumechoka kelele kila kukicha.